Mukhtasari wa Habari @ 1pm Waumini wa dini ya kiislamu kutoka - TopicsExpress



          

Mukhtasari wa Habari @ 1pm Waumini wa dini ya kiislamu kutoka maeneo mbali mbali humu nchini na ulimwengu kwa jumla wanasherehekea siku kuu ya Idd ul Fitr baada ya kukamilisha siku thelathini za mwezi mtukufu wa Ramadhan. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Naibu mkurugenzi wa mbuga ya wanyama pori ya Tsavo Mashariki na Tsavo magharibi capt. Robert Obrien amesema kuwa usalama wa wanyama pori kwenye mbuga hiyo umeimarishwa kikamilifu kwa muda wa mwezi mmoja ikilinganishwa na hapo awali. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Wapelelezi kutoka taifa la Marekani FBI na wenzao wa kikosi cha Israeli Mosaad wamejumuishwa kwenye kikosi kinachochunguza mkasa wa moto uliozuka katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jumatano wiki hii. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Watu wanne wamefariki huku wawili wakinusurika kifo baada ya ndege ya kijeshi ya Ethiopia ya kubeba mizigo kutua ghafla na kushika moto katika uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Posted on: Fri, 09 Aug 2013 09:49:41 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015