Mukhutasri mwa MWENGE WA SHEKI NA JOSEPH JIRA. Mwanamke mmoja - TopicsExpress



          

Mukhutasri mwa MWENGE WA SHEKI NA JOSEPH JIRA. Mwanamke mmoja raia wa Kenya anazuiliwa na maafisa wa polisi baada ya kupatikana na kilo nne za dawa za kulevya aina ya Heroin katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi hapa Mombasa. Mwanaharakati Okiya omutata amewasilisha ombi mahakamani akitaka jopo linalosuluhisha mizozo katika tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC lizuiliwe kutoa uamuzi iwapo Kethi Kilonzo na Philip Kaloki wanafaa au hafa kugombea wadhifa wa useneta katika kaunti ya makueni. Aliyekuwa waziri Raphael Tuju amehojiwa na maafisa wa polisi kuhusiana na kifo cha mwanamme anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe Ruth Akinyi. KIMATAIFA Ndege iliyokuwa ikimbeba rais wa Somalia Hassan shekh Mohamoud imelazimika kutua kwa ghafla mjini Mogadishu nchini humo. Ungana NA JOSEPH JIRA SAA KUMI ALASIRI KWA MWENGE MZIMA WA SHEKI
Posted on: Mon, 08 Jul 2013 11:51:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015