Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,Freeman - TopicsExpress



          

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA,Freeman mbowe amesema kuma waliohusika katika kitendo cha ulipuaji wa bomu katika uwanja wa soweto jijini Arusha ni kikundi cha watu na wala sio mtu mmoja. Mh Freeman ameyasema hayo leo majira ya saa 9:50 alasiri wakati akitoa salamu zake katika ibada ya mazishi ya katibu wa chadema katika kata ya sokon 1 jijin arusha bi Judith wiliam aliyefariki kutokana na mlipuko uliotokea hivi karibuni jijini hapa. Ameendelea kwa kusema kwamba kato hawatotoa ushaidi kwa polisi wa aliyehusika katika kulipua bomu siku ya jumamosi ya tarehe 15 mwezi huu kwa sabab polisi hao ni watuhumiwa. Hata hivyo mhe.MBOWE amemtaka raisi wa jamhur ya mungano wa Tanzania mh. JAKAYA KIKWETE kuunda tume huru ya mahakama itakayosikiliza madai hayo kwa uwazi na ukweli. NA HUMPHREY JOSEPH NIKIWA KATIKA KANISA LA KKKT DAYOSISI YA KASKAZIN KATI MTAA WA SOKON 1 JIJIN ARUSHA
Posted on: Thu, 20 Jun 2013 13:10:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015