Nawashukuru sana ndugu zangu wote kwa salamu za siku ya kuzaliwa. - TopicsExpress



          

Nawashukuru sana ndugu zangu wote kwa salamu za siku ya kuzaliwa. Jana nimesherekea siku ya kuzaliwa kwa namna ya kipekee kabisa kwa maisha yangu mpaka sasa. Siku moja kabla ya kufika kwa tarehe yangu ya kuzaliwa nilipata taarifa kuwa mke wangu amabaye alikuwa ni mjamzito hali yake imebadilika sana. Baada ya mawasiliano na daktari wake ambaye yupo Mwanza na kupewa majibu ya vipimo akashauri ni vyema kama atakutana nae mampema siku inayofuata kwa uchunguzi zaidi lakini itabidi kuwahi kwani siku hiyo hiyo mchana anasafari ya kikazi kwenda Arusha. Nikafanya jitahada mbalimbali hatimaye nikafanikiwa kupata Ndege ya mapema saa1 asubuh kutoka Bukoba. Mungu akabariki akafika salama Mwanza na kukutana na Daktari wake na baada ya kumchunguza na kumpima tena ikaonekana hakuna jinsi tukichelewa tunaweza kupoteza wote ( yaani mama na mtoto aliye tumboni). Baada ya uamuzi huo ikabidi operation ifanyike na Ninamshukuru mungu wamefanikiwa kuokoa maisha ya mama (mke wangu) na mtoto wa kiume, ingawaje hali ya mtoto bado haijaimarika kutokana na kwamba alikuwa bado ( pre mature) kama wiki 4 -5 kukamilika. Kwa sasa mtoto anasaidiwa na mashine ya Oxygen lakini tunashukuru Mungu kanazidi kuchangamka. Namshukuru mungu kwani nitakuwa ninasherehekea siku moja ya kuzaliwa na my new baby boy. MUNGU BARIKI FAMILIA YANGU. AMEN
Posted on: Thu, 29 Aug 2013 07:53:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015