Ndoto Kwa nini tunaita ndoto Wengi wetu tumawahi kuota ndoto - TopicsExpress



          

Ndoto Kwa nini tunaita ndoto Wengi wetu tumawahi kuota ndoto usingizini, picha halisi ya ile ndoto unakua nayo wewe kichwani, hata ukijaribu kusimulia, watu wataelewa ila sidhani (haiwezekani) kupata exactly picha ile ile ulionayo wewe kichwani mwako. Vivyo hivyo, katika ndoto zetu za kawaida kuhusiana na maisha, malengo, kuna picha unayokua nayo kichwani, wewe peke yako ndo unapicha halisi ya kitu unachokitaka kukifanya au kukiaccomplish. Unaweza kuwashilikisha watu, lakini jua kua wewe ndo unapicha kamili ya kitu gani unataka kitokee. *Pia mzigo wa kukitekeleza hicho kitu unatofautiana kutoka kwako mpaka kwa mwingine unaemsimulia maana wewe ndo mwenye picha hiyo halisi. *Pia jua kua uwezo wa kudaka/kuelewa kiitu unatofautiana kutoka kwa mtu moja au mwingine *Shauku ndani ya mtu ya kutaka hicho kitu kitokee inategeea mambo yafuatayo -umuhimu wa hiyo ndoto kwa huyo mtu. Hapa unaweza labda kua na ndoto ya kuinua soka la Tanzania, ukimfata mtu ambae ndani yake hana interest kabisa na mpira, nay eye ndani yake anapenda kuigiza, hata kama amepata picha nzuri kabisa ya kitu unachotaka kukifany, na akajua faida za hicho kitu katika kuleta mabadiriko, lakini kwa sababu hicho kitu hakina umuhimu saana katika maisha yake, hata kama ataku support, mchango wake hautakua wa hali ya juu kama ambavyo ungempa case ya uigizaji, hii ni kwa sababu yeye mwenyewe hana hamu saana na hicho kitu. Kitokee au kisitokee kwake ataona sawa tu na aisha yataendelea mbele. Hivo basi, wakati unachagua watu wa kuwashirikisha ndoto zako, uobe Roho takatifu akuongoze kwa watu ambao watakua wanapenda -Picha aliyoipata baada ya kusimuliwa hiyo ndoto. Kama picha alioipata ni hafifu na haijitoshelezi, atkua na msukumo kidogo au asiwe nao kabisa katika kuona ndoto inatimia. Zipo nyingi, ila pia tungependa kusikia zaidi kutoka kwenu, kama unazo nyingine ongezea…! Share and like it ili iwafikie wengi. Ubarikiwe
Posted on: Tue, 30 Jul 2013 09:56:07 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015