OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA - TopicsExpress



          

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI. SIMU: 2757083 SHULE YA SEKONDARI MWIKA, FAX: 2289573 S. L. P. 1945, MOSHI. Kumb: Na. MWSS/SA/2013 TAREHE …15/07/2013…………………………… Mwanafunzi, ………………..……………….. …………………………………. YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI MWIKA WILAYA YA MOSHI FORM (V) MWAKA ----2013------------------- 1:0: Ninafurahia kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga na kidato cha …………………………… katika shule hii mwaka …………………………… Shule hii iko umbali wa kilomita 43 kutoka Moshi Mjini barabara ya Moshi – Rombo Kutoka Mwika sokoni ipo mita 200 upande wa kaskazini mwa soko. Muhula wa kwanza wa masomo utaanza tarehe …29/07/2013 Unatakiwa kuripoti Shuleni kuanzia tarehe 29/07/2013. na mwisho wa kuripoti ni tarehe 05/08/2013 2:0: Mambo muhimu ya kuzingatia 2:1: SARE YA SHULE. (a) Wavulana – suruali mbili (2) za heshima za rangi ya kijani kisichoiva zenye marinda mawili, mashati mawili (2) meupe ya mikono mirefu, tai ndefu na sweta vinavyofanana rangi na kitambaa cha suruali. (b) Wasichana – sketi mbili (2) ndefu za kufunika magoti za rangi ya kijani kisichoiva zenye marinda boksi moja kubwa mbele na nyuma, mashati mawili (2) meupe ya mikono mirefu, tai na sweta vinavyofanana rangi na kitambaa cha sketi. VIATU: Kwa wote wavulana na wasichana – viatu vyeusi vya kamba visivyo na visigino virefu SOKSI: Nyeusi (pair) 2 kwa wavulana. Nyeupe (pair) 2 kwa wasichana. (c) Wasichana hawataruhusiwa kusuka nywele wakati wote wakiwa shuleni. NB: (i) Kitambaa cha suruali na sketi kimeambatanishwa. (ii) Sare ziletwe kukaguliwa siku ya kuripoti Mwanafunzi. 3:0: SHERIA NA KANUNI ZA SHULE HII. 3:1: Shule inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na Wizara yenye dhamana ya Elimu nchini. Unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo ambayo yatafafanuliwa kwa maandishi na utapewa nakala yake mara baada ya kuripoti shuleni. a) Heshima wa viongozi, wafanyakazi wote, wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla ni jambo la lazima. b) Mahudhurio mazuri katika kila shughuli ndani na nje ya darasa ni muhimu. c) Kutimiza kwa makini maandalio ya jioni (preparation) kwa wanafunzi wa hosteli. d) Kuwahi katika kila shughuli za shule na nyingine utakazopewa. e) Kufahamu mipaka ya shule na kuzingatia kikamilifu maelekezo ya kuwepo ndani na nje ya shule mipaka hiyo wakati wote wa uanafunzi wako katika shule hii. f) Kutunza usafi wa mwili na mazingira ya shule. g) Kuvaa sare ya shule wakati wote unapotakiwa. h) Kuzingatia ratiba ya shule wakati wote. i) Wanafunzi wakike hawaruhusiwi kusuka nywele wakati wote wakiwa shuleni. 3:2: Makosa yafuatayo yanaweza kusababisha ukafukuzwa shule. 1. Wizi 2. Uasherati na ushoga 3. Ubakaji 4. Ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya kama vule bangi, cocaine, mirungi, kuberi n.k 5. Kupigana na kupiga 6. Kuharibu kwa makusudi mali ya umma 7. Kudharau Bendera ya Taifa 8. Kuoa ua kuolewa 9. Kupata mimba au kuharibu mimba ndani na nje ya shule 10. Kutoa mimba 11. Kuchochea na kuongoza migomo au kuvuruga amani na usalama wa shule au watu 12. Kukataa adhabu halali kwa makusudi 13. Mwanafunzi kuwa na simu ya mkononi. 4:0: MAMBO MENGINE MUHIMU. a. Medical Examination Form ambayo itajazwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Serikali. Fomu hii itakabidhiwa kwa Mkuu wa shule au Msaidizi mara utakaporipoti shuleni. b. Fomu ya maelezo binafsi kuhusu historia ya mwanafunzi/mkataba wa kutoshiriki katika migomo, fujo na makosa ya jinai. c. Fomu ya mzazi kukiri kukubaliana na sheria, kanuni na taratibu za shule kama, kulipa ada, michango na maelekezo mengine yatakayotolewa na shule. 5:0: Tafadhali soma kwa makini maelekezo/maagizo haya na kuyatekeleza kikamilifu. MAHITAJI MENGINE KWA WANAFUNZI WA BWENI TU. 1. Shuka mbili (2) rangi ya kijani, mto na foronya, taulo, toileti paper (pieces 10), mswaki, dawa ya meno, blanketi 1 rangi ya kijivu, ndoo ya plastiki, madaftari makubwa ya kutosha, peni, samani za hisabati (Mathematical set). 2. Suruali nyeusi isiyobana kwa ajili ya kutumia darasani wakati wa usiku, bukta 2 za michezo rangi ya bluu/nyekundu, raba kwa ajili ya michezo, sketi mbili yeusi za tetron ziwe na marinda, t-shirt 2 bluu/nyekundu (kwa wasichana). 3. Suruali 2 nyeusi kwa ajili ya kazi za nje, bukta 2 za michezo rangi ya bluu/nyekundu, raba kwa ajili ya michezo, t-shirt 2 bluu/nyekundu (kwa wavulana). 4. Godoro lenye ukubwa wa f “2½” kwa f” 6” na unene wa inchi “4”. NB. Nguo zingine zisizoainishwa hazitakubaliwa. 5:1: ADA NA MICHANGO YA SHULE. S/N MALIPO MUHULA MWAKA 1 Karo ya shule 35,000/= 70,000/= 2 Nembo 2,000/= 2,000/= 3 Uboreshaji taaluma 10,000/= 10,000/= 4 Dawati 15,000/= 15,000/= 5 Kitambulisho 5,000/= 5,000/= 6 Ulinzi 5,000/= 5,000/= 7 Ukarabati wa majengo 25,000/= 25,000/= 8 Tahadhari 5,000/= 5,000/= 9 Huduma ya kwanza 5,000/= 5,000/= JUMLA 107,000/= 142,000/= MALIPO YOTE YALIPWE BENKI KWA AKAUNTI YA SHULE NA. 4031100215 NMB KWA KUANDIKA JINA LA MWANAFUNZI NA KIDATO ANACHOSOMA NA AJE NA RISITI (BANK PAY – IN-SLIP) ANAPORIPOTI SHULENI. FEDHA TASLIMU HAZITAPOKELEWA SHULENI – REJEA WARAKA NO. 13 WA ELIMU 2009. MAHAFALI: Mchango wa kila mahafali utatolewa mwezi mmoja (1) kabla ya mahafali yenyewe. 5.2: VIFAA VYA USAFI A: Ndoo moja plastiki ya lita 20 B: (i). Wavulana waje na: 1) Jembe 2) Hard broom (ii). Wasichana waje na: 1) Drier (moper) za kudekia 2) Panga KARIBU SANA KATIKA SHULE HII ………………………………………… D. P. GWALTU MKUU WA SHULE. Nakala: 1. Katibu tawala (M) Mkoa wa Kilimanjaro S. L. P. 3003, MOSHI. 2. Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, S. L. P. 3003, MOSHI. 3. Mwenyekiti wa Bodi, Shule ya Sekondari Mwika, S. L. P. 1945, MOSHI. FOMU YA UTII WA SHERIA NA TABIA NJEMA. Mimi……………………………………………………………………(jina kamili) kidato cha…………………………………. Mwaka ……………..ninatambua wajibu wangu kwa Taifa kama mwanafunzi na ninaahidi: a) Kwamba nitatii na kuwaheshimu viongozi wangu wote kuanzia ngazi ya monitor, viranja, walimu, watumishi wote hadi mkuu wa shule. b) Kwamba nimezisoma na kuzielewa na nitafuata sheria na kanuni zote za shule pamoja na maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na uongozi wa shule. c) Kwamba sitatoka nje ya shule wakati wa masomo labda tu kwa shughuli maalumu na baada ya kupata kibali kutoka kwa mwalimu au mkuu wa shule mwenyewe. d) Kwamba kama nitashindwa kufuata hayo yote hapo juu, hatua kali zichukuliwe dhidi yangu ambapo ni pamoja na kusimamishwa masomo. Tarehe…………………………………………….. ……………………………………………………… Jina na sahihi ya Mwanafunzi Tarehe ……………………………………………. ……………………………………………… Jina na sahihih ya shahidi Mzazi/Mlezi Tarehe……………………………………………. ………………………………………………… Sahihi ya Mkuu wa Shule. FOMU YA KUJIANDIKISHA SHULENI. A. HABARI ZA MWANAFUNZI. 1. Jina kamili (kama kwenye mtihani) ………………………………………………………………………………………………………………………………. 2. Tarehe ya kuzaliwa ……………………………………………… Dini ……………………………………….. 3. Mahali na wilaya aliyozaliwa …………………………………………………………………………………. 4. Shule aliyomaliza kidato cha nne…………………………………………………. 5. Masomo anayopendelea (i) ………………………………………… (ii) ………………………………….. (iii) ………………………………………………. 6. Kazi yoyote aliyowahi kufanya kama vile kiongozi wa michezo, kwaya, ngoma, kiranja, maktaba n. k. ……………………………………………………………………………………………………………… 7. Mambo unayopendekele kufanya nje ya masomo (kama michezo, ushonaji) (i). ……………………………………………………. (ii) …………………………………. (iii) ………………………… 8. Ninathibitisha kwamba habari zilizotolewa ni kweli na sahihi. Jina la mwanafunzi …………………………………………….. sahihi ………………………. Tarehe ………………… B. HABARI ZA MZAZI/MLEZI. 1. Jina kamili la baba ………………………………………………………………………………… yupo hai/amefariki. 2. Kazi yake …………………………………………………………………………………………………………………………….. 3. Jina kamili la mama ………………………………………………………………………………. Yupo hai/amefariki. 4. Kazi yake …………………………………………………………………………………………………………………………….. 5. Jina kamili la mlezi (iwapo mtoto haishi na wazazi wake) …………………………………………………… 6. Kazi ya mlezi/Mzazi …………………………………………………………………………………………………………… 7. Namba ya simu ya mzazi/mlezi ………………………………………………………………………………………….. 8. Anuani ya mzazi/mlezi ………………………………………………………………………………………………………… 9. Mtoto anaishi na (i) Baba (ii) mama tu (iii) wazazi wote (iv) Mlezi (kata isiyohusika) 10. Taja ndugu sita wa karibu wanaoruhusiwa kumtembelea mwanafunzi awapo shuleni. JINA NAMBA ZA SIMU/ANWANI UHUSIANO 1 2 3 4 5 6 11. Mimi ……………………………………………….. Baba/Mlezi wa ………………………………………………………….. Nathibitisha kuwa taarifa hiyo hapo juu ni sahihi na naaahidi kushirikiana na walimu ili kuhahikisha kwamba kijana wangu anakuwa na tabia nzuri, mchapa kazi na mwenye bidii ya masomo. Jina la Mzazi/Mlezi …………………………..…………………. sahihi …………………….. tarehe ………………….
Posted on: Thu, 18 Jul 2013 11:16:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015