Ofisa wa siasa za mambo ya nje wa umoja wa nchi za Ulaya bibi - TopicsExpress



          

Ofisa wa siasa za mambo ya nje wa umoja wa nchi za Ulaya bibi Catherine Ashtona amesema anatafuta uwezekano wa kutoa misaada ya Ulaya kwa Misri katika ziara yake nchini Misri ambayo imeanza jana. Katika maelezo yaliyotolewa na ubalozi wa Ulaya jijini Cairo imesema kuwa bibi Ashton atakutana na raisi Mohamed Morsi, waziri wa mambo ya nje Mh. Mohamed Kamel Amr na baadhi ya mawaziri na wawakilishi wa upinzani. Bibi Ashton pia anatarajiwa kushughulikia maendeleo ya hivi karibuni akijumuika na katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu katika ziara yake ya Mashariki ya Kati ambayo anatarajiwa kutembelea Jordan, Iraki, Lebanon, Misri, Israel na Palestina.
Posted on: Wed, 19 Jun 2013 13:25:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015