PENZI LA MTOTO WA MCHUNGAJI MTUNZI: PAUL NGIGWA THE STORY OF MA - TopicsExpress



          

PENZI LA MTOTO WA MCHUNGAJI MTUNZI: PAUL NGIGWA THE STORY OF MA LIFE SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE SIMU: 0762217077; 0655217077 MAIL-paul03.thegreat@gmail ****endelea**** Baada ya kuendelea kunywa pande zile kilaji kilinikolea mpaka saa tisa hivi jioni. Baada ya kujizoazoa pale baa nilikwenda moja kwa moja mpaka stendi na kukata tiketi kwenye gari ya Njombe ya Another G. Baada ya kukaa pale kwenye gari kwa muda kama dakika 15 hivi gari ilianza safari ya kwenda Njombe baada ya abiria kujaa kwenye ile gari. Mie nilikuwa siti ya mbele kabisa kwa dereva yaani jirani kabisa naye na kale kasiti kadogo kuna mtu alikaa pale katikati. Baada ya kufika njiapanda ya Tosamaganga yule abiria aliyekuwa amekaa kwenye ile siti ya katikati kumbe alikuwa ni rafiki yangu ambaye tulisoma wote Mdabulo Secondari. Nadhani sikumwona kutokana na kuwa nilikuwa nimepombeka kidogo. Baada ya kusalimiana na rafiki yangu yule mkononi alikuwa na konyagi mizinga minne na mie akniuluza kama bado natumia maana ananikumbuka sana nilivyokuwa mdau wa konyagi nilipokuwa sekondari. Nilimuitikia kwamba mie damudamu ndipo akanipa miwili, mmoja nikawa nauchapa mlemle kwenye gari. Baada ya kufika Tananghozi tuliomba kushuka kwa ajili ya kupunguza kiasi cha maji mwilini na abiria waliokuwa ndani ya gari ile wakawa wanacheka sana. Baada ya kuendelea na safari rafiki yangu yule alikolewa sana na pombe ambapo alinipa eti ndo nauli ya basi kutoka Iringa mpaka Mafinga sh. 20,000/= na nikaifutikiza mfukoni. Baada ya kufika Mafinga huku tukiwa tumepombeka vya kutosha tulishuka garini na yule jamaa yangu akaniomba sana kuwa nimsindikize mpaka alipokuwa akifanya kazi demu wake ambaye alikuwa ni baamedi kwenye baa moja maarufu pale Mafinga. Unajua yule jamaa yangu alikuwa siku ile na hela sana maana alikuwa ndo anatoka kufanya kazi Ruaha mbugani. Sikusita, nilimkubalia ombi lake na baada ya hapo tulichukua taxi mpaka kwa hiyo baa. Baada ya kufika pale tukaanza kunywa na upya kabisa. **** mie nililewa sana lakini kiukweli kutokana na damu yangu kuwa kali nilikuwa bado na akili zangu safi tu. Baada ya kukaa sana pale baa na kunywa sana mpaka saa mbili na nusu hivi nilitaka kuondoka. Lakini kabla ya kuondoka nilikwenda msalani kwanza ili nikanawe uso nipate nguvu za kutembea mpaka stendi ili nichukue taxi mpaka nyumbani. Nilipofika msalani, niliosha uso wangu na nikahisi kama nimehumuka hivi ndipo nilipojua kuwa pombe sasa ipo kwenye damu. Baada ya kurudi pale baa nilikuta meza ikiwa imejaa pombe za kufa mtu. Nilianza tena kunywa yaani nilifakamia pombe balaa na kumbe kuna li-baamedi fulani linanilia mingo ili liniseti. Mie kugundua hilo nikaaga na yule rafiki yangu akanipa tena hela kama sh 15,000/= hivi eti kwa ajili ya taxi. Nilitoka na kuangaza macho huku na huko na baada ya kujihakikishia usalama nikaanza mdogo mdogo mpaka stendi. **** Nilifika stendi na kutaka kukodi taxi lakini nilighairi na nikaamua kwenda kwa mguu mpaka home. Nakumbuka pale nyumbani walikuwa wamewasha taa zote za nje, sebuleni na jikoni pamoja na chumbani. Ninachokumbuka sasa ni kuwa nilipofika getini nakumbuka zile taa za ulinzi nilinipiga usoni nikahisi pombe kunizidia. Baada ya kuona hivyo nikafumba macho na kuotea mlango ulipokuwa na nilipofika nilizima taa zote maana swichi ya taa zile ilikuwa pale mlangoni. Baada ya kukaa na kutulia kama nusu saa hivi sikuelewa kilichoendelea mpaka saa kumi na moja alfajiri niliposhtuka kutoka usingizini. ***Mdogo wangu Nelsony hapa akawa ananisimulia ilivyokuwa*** Unajua kaka ulikuja na kuzima taa zote hapa sebuleni na kwa bahati nzuri mzee alikuwa hajarudi bado hivyo ikawa sawia kabisa. Baada ya wewe kuonekana umepombeka sana kaka na kutokana na ulivyokuwa unapiga stori za hali ya juu sana na kwa sauti tulikusihi sana uende ukalale lakini ulikataa na ukadai kuwa utalala baada ya mzee kufika na unataka kuongea naye habari kadhaa. Baada ya muda ulipitiwa na usingizi sebuleni na mie na Zakayo(house keeper) tulikubeba ukiwa hujielewi mpaka chumbani mie nikakuvua nguo zote na kukulaza na ukalala fofofofofo. Baada ya hapo nilikuwekea chakula chumbani ili ukiamka ule na baada ya hapo mzee alipofika alituuliza uko wapi na tukamjibu kuwa umechoka sana na umeshalala. Ilipofika asubuhi ndipo tukaanza kucheka sana kutokana na mambo uliyokuwa ukiyafanya jana" alimalizia. **** Mie usiku ule saa kumi na moja ile niliamka na kujihisi uchovu, nilikwenda bafuni na kuoga na baada ya hapo nilirudi tena kulala. Saa mbili ndipo nilipoamka na kukuta wenzangu wakicheka sana kutokana na mambo ya jana ama kweli usilolijua ni kama usiku wa giza **** itaendelea kesho asubuhi na mapema kama kawaida. Twende pamoja wadau kama una lolote la kusema nami tupia na kama unataka iwe siri fanya kuni-inbox hivi.
Posted on: Mon, 22 Jul 2013 12:14:56 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015