PIGO KWA VYOMBO VYA HABARI Kwa mara yangu ya kwanza katika jarida - TopicsExpress



          

PIGO KWA VYOMBO VYA HABARI Kwa mara yangu ya kwanza katika jarida hii, ningependa kupinga ripoti ya kampuni ya utafiti ya Ipsos Synovate kuhusu vyombo vya habari. Kulingana na matokea yao ni kwamba vyombo vya habari imeshuka umarufu kutoka nambari moja hadi nne!. Kamwe haiwezekani maana bila vyombo vya habari hata ripoti enyewe haingejulikana. Kwa sasa rais anaongoza, akifuatiwa na naibu wake, huku viongozi wa dini wakishikilia nafasi ya tatu, kisha vyombo vya habari wakiorodheshwa wa nne. Vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kwa kuwatetea wanainchi, kuwafahamisha, burudisha, elimisha na kuandaa mada mbalimbali za majadiliano. Hakuna siku moja mwanafunzi akamshida mwalimu. Sasa Ipsos Synovate wanasema ni maoni ya waliohojiwa . Labda waliohojiwa hawaelewi jinsi vyombo vya habari hutekeleza majukumu yake. Sasa kuna mpango wa kulemaza wa vyombo vya habari na serikali. Mpango huu ni kudhibiti uhuru wa kutangaza na kupeperusha vipindi, taarifa za habari, habari za hivi punde, na mambo mengi ambayo huenda yakanyima wananchi haki zao za kupokea habari Kwa hivi sasa sheria zinaundwa kuhakikisha vyombo vya habari zitakuwa chini ya tume mpya ya mawasiliano(Communications Authority of Kenya) kutoka kwa ya zamani (Communications Commission of Kenya). Mabadiliko kama haya yatalemaza uhuru wa habari yawa kama yalivyo kabla ya mwaka 1998.(Communication Act 1998). Vyombo vya habari vinaweza kujimsamamia huku jopo la mawasiliano (Media Council of Kenya) wakisimamia upeperushaji wa vipindi vyote kama dastaru. Mpango huu huenda ukaanza kutekelezwa mnamo 27, Agosti, 2013. Tunaomba wakuu wa nyumba mbalimbali, wasimamizi, wakurugenzi,wahariri na wanahari wote wapinge mpango huu. Hata Ajuza wangu katetea kasemaaa: Mgala muuwe na haki yake mpe kwani pilipili usioila yakuwashia nini.
Posted on: Thu, 11 Jul 2013 13:32:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015