Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela bado - TopicsExpress



          

Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela bado anaendelea kuwa katika hali mbaya na hawezi kuzungumza kwasababu ya mirija ambayo inafanya mapafu yake yasiwe na majimaji, licha ya kuwa yuko katika hali ya utulivu. Mke wake wa zamani Winnie Madikizela Mandela ameliambia gazeti la Sunday Independent kuwa Mandela amekuwa katika hali ambayo anaweza kukabiliwa na maambukizi kwa haraka na kwa hiyo anapaswa kuwa katika hali ya usafi kila mara. Kutokana na mirija hiyo , amesema Winnie kuwa anaweza kuwasiliana tu kupitia uso wake. Ameongeza kuwa madaktari wamesema wanamatumaini ataweza kuzungumza, na kuongeza kuwa atapatiwa matibabu na madaktari 22 nyumbani kwake.
Posted on: Mon, 18 Nov 2013 10:33:21 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015