STORY ; KICHAA MWENYE - TopicsExpress



          

STORY ; KICHAA MWENYE AKILI,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,MTUNZI ; JUNIOR B;,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,SEHEMU YA TISA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,PHONE ; 0755957515,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Wazee wa jadi wamekutana ili kujadiliana cha kufanya ili kumkomoa Mzee Mwikwabe kutokana na malingo na dharau anazowaonesha juu ya tamaduni zao kutokana na kuwa na urafiki na Mwalimu Nyerer na pia mtoto wake kusoma, je watafanikiwa??????????????????????????????,,,,,,,,,,,,,,,endelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,naomba tutoe mawazo yetu ni namna gani tufanye ili kumfunza huyu Mzee?" aliuliza mkuu wao, " mimi nafikili tumuue tu" akashauri mzee wa kwanza," me nafikili tumuue mwanae anayemlingia" akashauri mzee wa pili, " mimi nafikili tumwangamize yeye na ukoo wake wote" akashauri mzee wa tatu, mawazo yalitolewa mengi sana ila baada ya kujadiliana kwa muda wakaamua kufanyia kzi wazo la kuteketeza ukoo mzima wake," naamin kila mmoja ameafiki wazo la kuungamiza ukoo wa mzee Mwikwabe ila tatizo tunauteketezaje?" akauliza mkuu wa wazee wale wa jadi," mimi nafikili haina haja ya kuuteketeza ukoo wake kirahisi, inabidi tumpe maumivu yatakayomfanya ajutie vitendo vyake" akashauri mmoja wao" sasa ni zamu ya kuushilikisha mzimu wetu uamue cha kufanya kwani maazimio yetu tumemaliza, " akasema mkuu wao, na pale pale wakachinja kafala ya kondoo mweupe kwa ajili ya kuuuita mzimu, wakafanya mzindiko yao na wakati wanaelekea kuyakamilisha kwenye mti wa mkuyu kati kati ukaanza kutoka moshi kidogo na kadri muda ulivyoenda ndivyo ulivyozidi kuwa mwingi, radi kali zikawa zinapiga mahali pale, ikumbukwe kuwa radi na mvua au ngurumo za mzimu zilisikika pale kwenye matambiko pekee ingawa zilikuwa na kelele kubwa sana" hahahahahahahahaha!!!! Hahahahahahahahahahaha! Ombi lenu nimelisikia!!! Ombi lenu nimelisikia!!!!! Nitalifanyia kazi!!!!! Nitalifanyia kazi!!!" ilisikika sauti kali kutoka katika ule moshi, na ghafla ule moshi ukakatika na mzimu ukawa umeshaondoka, wazee wale wakamalizia tamaduni zao na kurudi makwao wakisubiri mzimu ufanye kazi,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mwita Mwikwabe aliendelea na masomo yake vizur akisubiri kuingia JKT na baadae kwenda Ulaya kusoma kama mwalimu alivyomuahidi baba yake, siku moja ameamka alisikia kichwa kinamgonga sana, akaamua kutoingia darasani na kupumzika chumbani, baadae mida ya saa tatu akaamua kwenda nje ya shule ili akachukue dawa kwa kuepuka kwenda kwenye dispensar ya shule ambako wangetaka akapimwe kwanza ndo baade apewe dawa zisizo na viwango, akanunua dawa na kuelekea mgahawa mmoja jirani na kuomba maji amezee dawa, mwisho akaona bora apumzike pale na kuagiza chai ili anywe, baada ya muda akaamua kurudi shuleni, alipofika getini akashangaa kukuta gatini pamefungwa na kuna skauti wa shuel nao bila kupoteza muda wakamweka chini ya ulinzi," kuna nn? Jaman! Mbona sijawaelewa?" akajitutumua kuuliza" ndg unatafutwa kama jambazi, ndo maana geti limefungwa kwa ajili yako, kuna wizi humo ndani na wewe ndiye mtuhumiwa" skauti mmoja akamwambia, ki ukweli alishangaa ila kwa kuwa hakuwa na jinsi ikabidi atulie, wakamchukua na kwenda naye mpaka ofisi za shule, akakuta walimu wapo katika kikao hivyo ikamlazim asubiri mpaka kikao kiishe, alikaa pale muda mrefu na baade akaruhusiwa kuingia kwenye kile kikao, akakalisha kati kati na maswali yakaanza" Mwita?" akaita mwalim wa nidham," naam mwalim!" akaitika kwa nidham," ulikuwa wap? Na kwa nini hujaingia darasani?" mwalimu akamtupia swali," nilijisikia naumwa asubuhi ndio maana sikuingia darasani na nilikuwa hapo center kununua dawa" akajibu kwa kujiamin," uliomba ruhusa ya kutoingia darasani kwa nan? Na ya kwenda nje kwa nan?" mwalim akaendelea na maswali," mmmm! Si mtu" ilimuwia vigum kujibu hilo swali ila akajalib bila kujua kuna nn?" unajua juu ya upotevu wa shiling sabini na senti kumi na saba pamoja na kaptula tatu na shati nne za wanafunzi unaoishi nao chumba kimoja asubuhi ya le?" mwalim akauliza huku akitoa taarifa,alishangaa kwa muda akiwaangalia walim wote kwa zamu na baadae akajib" sijui",walim wakamwangalia kwa muda kisha " tukisema kuwa wewe ndiye uliyeviiba hivyo vitu na kwenda kuviuza mtaani tutakuwa tunakosea?;,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,je ni kweli kaiba yeye??????????????????????????atafanywaje???????????????????usikose kesho!8-)
Posted on: Mon, 29 Jul 2013 19:24:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015