STORY: SITAISAHAU DAR ES SALAAM MTUNZI: MKWELI WA KITAA MHARIRI: - TopicsExpress



          

STORY: SITAISAHAU DAR ES SALAAM MTUNZI: MKWELI WA KITAA MHARIRI: COX DAWA YAO #ILIPOISHIA Nilijikuta nashindwa kupokea simu na kushindwa kumjibu mzee Mbingi swali lake, #SASA_ENDELEA SEHEMU YA AROBAINI NA TATU -43 .. ...nilikuwa naingalia tu ile simu kwani sikuwa najua cha kumjibu, ikanibidi niipokee ile simu kwani nilihisi ninaweza kumfanya Mzee Mbingi awe na wasiwasi kuhusu ile simu, Nilipoipokea nilisikia sauuti ya Rahma ikipenya kwenye ngoma za masikio yangu kwa ufasaha kabisa, nilimsikia Rahma akilalamika ""uko wapi jamani, au niambie upo wodi gani nikufuate!? Nilijikuta kwenye wakati mgumu sana kumjibu Rahma hatimae nikaona nimjibu, nikamwambia "" nisubiri nakuja sasa hivi"" Kisha nikakata simu Nilianza kuwaza kuhusu Rahma huku mzee Mbingi akiniangalia kama mtu anayetaka kuniuliza kitu kisha akawa ananiangalia akisubiri nimueleze jambo lolote, Wale waliongia kumuangalia mgonjwa Wakawa wametoka hivyo tukawa wote tupo pale nje tunajadili jadili kuhusu baadhi ya dawa ambazo daktari alisema kuwa hazipo pale hospitali na inabidi zikanunuliwe duka la pale nje ya hospitali, Bahati nzuri mzee Mbingi na mama mkwe pamoja na yule mama walichanga kiasi cha pesa na kunikabidhi mimi ili niende nikazinunue hizo dawa hapo nje ya hospitali, Haraka haraka nikachukua zile fedha na kuanza kuelekea nje ila nikakumbuka kuwa nimesahau kikaratasi chenye maelekezo ya hizo dawa, nilirudi haraka na kwenda kukichukua kile kikaratasi na kwenda nje ya hospitali kununua zile dawa, Nilipofika pale kwenye lile duka nilimpa kikaratasi pamoja na zile hela yule dada aliyekuwepo pale kwenye lile duka kisha nikatoa simu mfukoni ili nimpigie Rahma na nionane naye, Nilitoa simu mfukoni nikampigia Rahma na kumuelekeza duka nililokuwepo kisha akanijibu kuwa yeye hayupo mbali na pale na tiari ameliona hilo duka, Niliamua kukata simu kwani aliniambia anakuja pale fasta, Yule dada aliyekuwa anauza dawa kwenye ile phamarcy aliniambia kuwa dawa zangu zipo tiari na akaandika baadhi ya maelezo kwenye vile vipakiti kisha vyote kwa ujumla akaviweka kwenye mfuko wa rambo na kunikabidhi, Nilistushwa na mikono laini iliyotokea kwa nyuma yangu na kuniziba macho yangu huku mule ndani kukitawaliwa na harufu nzuri ya malashi ambayo mpaka leo sikujua ni manukato ya aina gani kwani yalikuwa yananukia vizuri sana, nilitumia nguvu kidogo kutoa ile mikono kwenye macho ndipo nilipokutana na uso mzuri wa mtoto Rahma, Rahma aliachia tabasamu la kujilazimisha na kunisalimia huku dimpozi zake zikionekana vizuri sana, Kwakweli Rahma aliamsha hisia zangu kabisa ila nikakumbuka kuwa nimeagizwa dawa, ikaninibidi nitoke na Rahma mpaka nje ya lile duka la dawa kisha nikamueleza hali halisi kwa haraka haraka na nikamuambia anisubiri pale pale fasta,Rahma hakutaka kunisubiri na akaniambia kuwa yeye yupo kwenye hatari na ingekuwa vizuri kama ningeongozana naye, Nilijitahidi sana kumuelewesha Rahma pale hadi akanielewa kisha mimi nikaanza kukimbia kurudi ndani ya hospitali kwa ajili ya kupeleka zile dawa, Nilifika mpaka nje ya wodi nikawakuta ndugu wa shemeji Chausiku,mama mkwe pamoja na Mzee Mbingi wakiwa wote wapo katika hali fulani ya majonzi kutokana na mgonjwa, nilimkabidhi mama mkwe zile dawa na kisha mama mkwe akampelekea daktari, Hali yangu kifikira na kimawazo haikuwa pale kabisa kwani muda wote nilikuwa namuwaza Rahma, nilijikuta mara nasimama mara nakaa kwenye benchi huku mzee Mbingi akiwa ananiangalia sana, Mzee Mbingi akaniita pembeni kisha akaniulizat, Mzee Mbingi:.. "unajua Rama, kwa huu muda mfupi niliokaa na wewe nimekuelewa baadhi ya tabia zako, hebu kuwa muwazi kijana wangu, nani aliyekupigia simu muda ule wakati tunakuja huku?, na ni nani uliyemuambia akusubiri kidogo kuwa utaenda kumfuata?"" Kwakweli nilishindwa kabisa kumjibu swali mzee Mbingi na nikabaki nimejiinamia, Wazo la kumueleza ukweli mzee Mbingi lilinijia huku nikishindwa pa kuanzia, kuna akili iliniambia nimuongopee mzee Mbingi lakini nikaona bora nimueleze ukweli kwani niliamini yeye ndo alishakuwa mzazi wangu kwa wakati huu, wakati nataka kumueleza Mzee Mbingi ukweli simu yangu iliita na nilipoiangalia alikuwa ni Rahma tena ananipigia, Niliamua kuipokea kwani niliamua kama lolote liwalo na liwe, nikamuambia Rahma ndo natoka aendelee kunisubiri pale pale kisha nikakata simu, baada ya kukata simu nikamuambia mzee Mbingi; MIMI:.. "ni stori ndefu sana mzee wangu, ila naomba unisamehe kwa kutokueleza mapema"" Nikamueleza mzee Mbingi hali halisi kwa ufupi kuhusu mimi na Rahma na matukio yote tuliyoyapata ila sikumuambia kuwa nilishawahi kufanya mapenzi na Rahma, Mzee Mbingi alinisikiliza kwa umakini sana kisha akaniambia ""nimekuelewa Rama, ila nakushauri nenda naye mpaka nyumbani kisha musitoke mpaka mimi nije kwa ajili ya usalama zaidi, ila kuweni makini sana"" Baada ya kunieleza vile mzee Mbingi aliingiza mkono mfukoni na kutoa elfu mbili (2000/=) na kuniambia kuwa nifanye kama nauli, Nilimshukuru sana mzee Mbingi kwa busara zake kisha nikamuaga na kutoka eneo lile huku ndugu wengine wa Chausiku pamoja na mama mkwe wakiniangalia sana, Nilitoka mpaka pale nje ya hospitali na kwenda mpaka pale nilipomuacha Rahma lakini sikumuona, Nilianza kupatwa na wasiwasi na kutoa simu yangu mfukoni ilinimpigie, nilipompia niliambiwa kuwa simu yake haipatikani Mawazo ya kwamba Rahma ametekwa yalianza kuniingia kwa kasi kichwani mwangu, nikaenda mpaka kwenye lile duka nililoenda kununua dawa na kumuulizìa yule dada lakini naye aliniambia kuwa tangu nilipotoka naye mida ile hakurudi tena, Nilianza kupatwa na wasiwasi na akili yangu ikanituma nirudi ndani ili nikamueleze Mzee Mbingi.... Itaendelea kesho Gonga LIKE kama umeipenda SPONSORED BY: #MARTHA_SHIJA_LAURENT KAMA UNATAKA KUIDHAMINI HII STORY TAFADHALI NI-INBOX KWANI LEO DADA YETU #MARTHA NDO ALIYESIMAMIA SHOW
Posted on: Wed, 31 Jul 2013 18:05:22 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015