SURA YA TISA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO SEHEMU YA KWANZA KUUNDWA - TopicsExpress



          

SURA YA TISA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO SEHEMU YA KWANZA KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO 105.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano. (2) Wajumbe wa Bunge watakuwa wa aina zifuatazo: (a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi; (b) Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa Washirika wa Muungano. (3) Kwa madhumuni ya Ibara ya ndogo (2)(a), kila mkoa kwa upande wa Tanzania Bara na wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni jimbo la uchaguzi. (4) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme. (5) Wabunge wote katika kila Jimbo la Uchaguzi watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina sheria inayoweka utaratibu kuhusu mambo ya uchaguzi. 106.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, maisha ya kila Bunge yatakuwa ni muda wa miaka mitano. (2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), maneno "maisha ya Bunge" maana yake ni muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge Jipya litaitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa wabunge na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha uchaguzi mwingine kufanyika. 107.-(1) Bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano chenye madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii. (2)Katika kutekeleza majukumu yake, Bunge litakuwa na madaraka yafuatayo: (a) kujadili na kutoa ushauri katika mambo yote yenye maslahi 108.-(1) Katika kutekeleza madaraka ya kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba hii, wajibu wa Bunge itakuwa nikuishauri Serikali na endapo Bunge halitaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa suala lililotolewa ushauri, basi Bunge litakuwa na haki ya kuiwajibisha Serikali kwa mujibu wa madaraka iliyopewa katika Katiba hii. (2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1), Bunge halitachukua hatua yoyote ya kiutendaji ambayo, kwa desturi ni shughuli za Serikali, na halitatoa maagizo yoyote ya kiutendaji kwa Serikali na Watumishi wa Umma, isipokuwa Bunge litashauri kuhusu suala lolote lililo katika dhamana ya Waziri anayehusika. 109.-(1) Mamlaka ya kutunga sheria juu ya mambo yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano yatakuwa chini yaBunge. (2) Mamlaka ya kutunga sheria katika Tanzania Bara na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yatakuwa chini ya Bunge la Tanzania Bara na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. (3) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka. (4) Endapo sheria iliyotungwa na Bunge la Tanzania Bara au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano, sheria hiyo itakuwa batili na itatenguka. (5)Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Tanzania Bara naKatiba ya Zanzibar, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri ya Muungano kwa mambo yanayohusu Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, basi sheria hiyo nyingine, kwa kiasi kinachokiuka Katiba hii, itakuwa batili.....
Posted on: Fri, 30 Aug 2013 09:56:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015