Si jambo baya ila kwa namna linavyofanyika, hakika tunatia aibu - TopicsExpress



          

Si jambo baya ila kwa namna linavyofanyika, hakika tunatia aibu kwani inaonesha ni jinsi gani tulivyojaa unafki wa hali ya juu nafsini mwetu. Eti kwa sababu ya ujio wa Obama jiji zima halijatulia, eti watu ndo wanafanya usafi maeneo muhimu kama kupaka rangi, kuotesha maua, kufagia takataka, kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo ktk maeneo yao ya kila siku, kukagua magari mabovu barabarani n.k n.k. Mimi binafsi naona haijakaa sawa kwani tunaonesha unafki na ushenzi wa hali ya juu. Je ina maana siku hizo zote serikali haikuwahi kuona kuwa yanayofanywa sasa yangepaswa kufanyika kila siku kama sehemu ya maisha yetu? Hapa tunamdanya nani hasa? Sisemi kuwa kufanya usafi ni vibaya la hasha, ila namna serikali yetu inavyotilia mkazo wa mambo fulani kuendana na matukio inaonesha ni serikali dhaifu namna gani tuliyonayo. Inatia hasira sana na kichefuchefu hasa pale wamachinga wanapobomolewa vibanda vyao na kufukuzwa hata kupigwa kama mbwa eti wako maeneo hayo kinyume na sheria. je, ni leo ndio serikali inaona hayo? Hao wamachinga kwani wameanza kufanya biashara zao maeneo hayo leo? Ni kwa nini tunakuwa busy tu wakati viongozi wa nchi tajiri wanapokuwa wanakuja nchini? kwa nini isiwe hivyo pia kwa kila raisi anayekuja nchini bila kujali ametokea wapi kama hasa ndiyo mikakati ya serikali yetu? Au kwa sababu tunaogopa tusiposafisha jiji na kuficha uozo na uchafu wetu hatutapata kitu tena toka huko kwa matajiri? Mimi nafikiri hii ndio sababu kubwa serikali kufanya hivi; kama sababu ni tofauti na hii basi ingefanya hata hivyo pale ambapo angekuja raisi madhalani wa Zambia. Hakika bado tuna safari ndefu sana; Tunatia aibu sana tena sana tu; Kwa aina hii ya utendaji, serikali inawajengea nini wananchi wake? Kama ni suala la usafi kwa nini siku tusiwe tunafanya hivyo siku zote kama sehemu ya mikakati ya usafi kama ambavyo inavyofanyika sasa?
Posted on: Thu, 27 Jun 2013 17:22:45 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015