Story: mke wa mtu **sehemu ya 13** mtunzi: - TopicsExpress



          

Story: mke wa mtu **sehemu ya 13** mtunzi: king junior **msimamizi: Kanye Kanyele Frank Masai** ** Aliponiambia kuhusu duka nilimshukuru kwa kunionyesha roho ya kunijali, akaniambia nia wajibu wake kutokana na raha nilizokuwa nikimpa na pia mimi kwake ni sawa na chemchem ya maji iliyoibuka katikati ya jangwa mbele ya mtu aliyekaribia kukata roho kwasababu ya kiu,,, Baada ya maongezi, wakati huo ilikuwa kama saa tatu, akaniambia yeye anaondoka hawezi kulala pale kwani mumewe angeweza kumtilia shaka kutokana na kwamba tangu mchana aliaga anaenda kwenye harusi ya rafiki yake. Sikumpinga japo nilikuwa natamani tulale wote hadi asubuhi ,lakini ni kitu ambacho kilikuwa hakiwezekaniki. Akatoa pesa kwenye mkoba wake na kunikabidhi huku akisisitiza kauli yake ya kunifungulia duka ili aweze kunifaidi vizuri bila kikwazo kutoka kwa mtu yeyote, kisha akaniaga na kuondoka. Alipoondoka nikahihesabu pesa ile ilikuwa ni laki moja. Sikutaka kuondoka usiku ule ikabidi nilale pale pale hotelini hadi asubuhi. Usiku niliwaza sana kuhusu maisha yangu ya baadaye yangekuwaje nikaona akinifungulia duka ndo muda muafaka wa kujipanga na kuoa ili niachane na wake za watu wazo nililoliona ni la muhimu sana kama litatekelezeka *** NILIJIDANGANYA*** Kesho yake asubuhi kulipopambazuka nikaamka na kuingia bafuni kuoga, nilipotoka nikajiandaa kisha nikelekea barabarani kusubiri daladala kwa ajili ya kuelekea kazini, ila nilikuwa nimechelewa japo si sana ila kama ujuavyo usafiri wa daladala jijini dar es salaam mida ya asubuhi ulivyokuwa wa shida sana. Nilikaa pale barabani kwa muda hadi kupata usafiri ikawa ni tabu sana kwani kila daladala ilikuwa ikija imejaa sana kiasi kwamba ikawa ni kero. Nikiwa nimekata tamaa, hatimaye nikapata usafiri na kuelekea kazini** Nilifika kazini muda ukiwa umeenda sana ila kwakuwa bosi alikuwa ni mpenzi wangu, hakunigombeza japo aliniuliza maswali ya hapa na pale nikayajibu kwa kumdanganya ili asijue kinachoendelea.Basi nikaendelea na kazi kama kawaida tena kwa bidii sana, sikutaka wafanyakazi wenzangu wajue kinachoendelea kati yangu na bosi wetu hivyo mara nyingi nilikuwa pamoja nao,, Siku hiyo ilipofika majira ya mchana kichwa kikaanza kuniuma sana hadi jasho likawa linanitoka, nikawa hata nguvu za kufanya kazi zikaniishia. Jackline(bosi) akaniambia niende hospitali ili nijue ni nini tatizo lakini nikamwambia hapana labda ni kutokana na kufanya kazi muda mrefu bila kupumzika, hivyo kitaacha tu muda si mrefu. Ikabidi niende dukani nikanunua hedex za kutuliza lakini hata nilipozimeza hazikunisaidia kwa lolote, badala yake zikawa kama ndo zinanizidishi maumivu, sijui ilikuwaje lakini wakati nanyanyua boksi la juisi kulitoa nje kwa ajili ya mteja ,nilihisi kizunguzungu kikali sana, nikashidwa kujizuia macho yakaanza kuona giza wakati ilikuwa ni mchana, nikaanguka chini kama mzigo sikujua kilichoendelea hadi nilipokuja kushtuka na kujikuta nipo juu ya kitanda huku nikiwa nimetundikiwa dripu ya maji. Nikagundua nipo hospitali, nilipogeuza macho yangu pembeni nikamuona Jackline pamoja na mwanaume mmoja wa makamo kiasi wakiwa wamekaa kwa pembeni. Walipoona nimezinduka Jackline akasimama na kusogea hadi pale kitandani na kuniuliza jinsi ninavyojisikia ,nikamwambia najisikia vizuri kiasi ila nahisi mwili umechoka sana. Nikamuuliza kwani ilikuwaje hadi nikawa pale hospitali nimetundikiwa dripu" akaniambia, walinikuta nimezimia hivyo wakanibeba na kunileta pale hospitali ya mwananyamala na nilipopimwa iligundulika kuwa nina malaria kali sana na nimezimia kwa siku moja, vilevile yule aliyekuwa amekaa pale pembeni ndiye mume wake, yule mwanaume akanipa pole, wakati tunaendelea na maongezi akaingia daktari na kuwataka waniache nipumzike kwani hali yangu haikuwa nzuri sana hivyo ilihitaji muda wa kupumzika,, basi wakatoka nje huku wakinihahidi kurudi baadaye kwa ajili ya kuangalia taratibu nyingine au jioni nitaruhusiwa baada ya wao kuondoka haikupita muda mrefu akaingia mtetezi wangu aliyenihahidi kunifungulia duka kiukweli alisikitika sana kwa hali yangu ile akaniambia huenda ni kazi bila mapumziko ya kutosha akanihahidi ndani ya wiki mbili niatkuwa nikimiliki biashara yangu mwenyewe nilizidi kumshukuru sana huku nikimsisitizia umakini juu ya mume wake asije akagundua kama tumenza tena mawasiliano kwani ingekuwa ni balaa kama alivyohahidi akaniambia pia dokta alivyomwambia kuwa kesho yake ningeruhusiwa kurudi nyumbani akaniambia kuwa na gharama zote atalipia tuliongea kwa muda hadi aliponiaga na kuondoka, jioni akaja Jackline katika mazungumzo akaniuliza kuhusu mtu aliyelipia gharama zangu kwani alipotaka kumlipa dokta akamwambia kuwa kuna mwanamke kazilipia *** nilibaki njia panda nisijue cha kumjibu kwani kama ningemwambia ni yule rafiki yake angeleta utata sana lakini ningemdanganya vipi hadi anielewe lakini sikuwa na jinsi nikamweleza mtu huyo ni nani kweli kama nilivyotarajia alikasirika sana nilijitahidi kumwel ewesha hadi akanielewa japo niliona kama hajaridhika lakini mi nikaona liwalo na liwe kwani yule alikuwa msaada mkubwa kwangu kuliko huyu**keshomajira kama ya saa nne kuna nesi mmoja aliniletea chai kiukweli nilimshukuru sana kwani hadi wakati sikuwa nimemwona mtu hata mmoja pale hospitali,,,,hadi inafika mchana kimya lakini ilipofika jioni akaja,,,,, itaendelea kesho saa 11 jioni
Posted on: Wed, 14 Aug 2013 16:25:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015