*Sugar Mamy* No 54 "Bwana wa Yehova - TopicsExpress



          

*Sugar Mamy* No 54 "Bwana wa Yehova ahimidiwe sana......"Dick aliongea kwa sauti kubwa "AMEEEEEEEEEEEEEN........"Wote wakaitikia kwa furaha "ALELUYAAAAAAAAA......."Dick aliongea tena kwa sauti ya juu zaidi "AMEEEEEEEEEEEN.........."Watu waliitikia kwa sauti ya juu zaidi "Nawashukuru sana Wananchi wa Kigoma kwa kutokuwa wagumu wa kusikia neno"Dick aliongea huku akizunguka kila pande ya jukwaa "Nawashukuru sana kwa mioyo yenu ya usikivu,,hivyo hivyo muwe wepesi katika kubadili maisha yenu"Dick aliongea huku watu wakimpigia makofi "Mmesikia ushuhuda wa #Sabina_Mwanga au #Mama_Ray japo wengi walikuwa wakimuita #Sugar_Mamy"Dick aliongea huku mama Ray akiwa pembeni amesimama na Nasra mke wa Dick "Lakini yote aliyoyafanya mama Ray yalikuwa na sababu zake"Dick aliongea huku akifuta jasho lililokuwa likianza kumtoka "Sababu ya yote ni kumfanya mama huyu kuwa chombo cha uponyaji,,chombo cha ubadilishaji maisha ya watu,,chombo kilichowafikia leo wananchi w KIGOMA na kubadilisha mioyo yenu iliyokuwa migumu kumpokea YESU"Dick aliongea kwa sauti huku kelele za makofi na vigeregere vikisikika!! "Mimi mwenyewe nilitaka kujiua mwaka wangu wa kwanza baada ya kusikia kuwa mama huyu niliyekuwa nafanya naye uzinzi kwa miaka miwili ameathirika kwa ukimwi"Dick aliongea na watu wote wakawa kimya wakimsikiliza "Lakini Mungu akasema hapana,,huwezi kufa kabla hujaenda kuwabadilisha watu wa KIGOMA"Dick aliongea "Huwezi kufa kabla hujawabadilisha watu wanaosoma stori hii iliyoandikwa na #HAJRAT"Dick aliendelea kutoa mifano iliyo hai "Basi Mungu akanifanya kuwa chombo cha kutangaza neno lake duniani kote"Dick aliongea huku akishangiliwa na mamia ya watu "Kwanini ujiue kwa kuwa muathirika.............?"Dick aliuliza kwa sauti ya juu "Je dawa ya Ukimwi ikipatikana kesho,,si itakuwa faida kwa aliyesubiri?"Dick aliuliza swali lililoonekana kuwaingia sana watu akilini "Ili uwe na moyo wa matumaini ni lazima uwe ndani ya YESU na usimruhusu shetani akupe moyo wa kukata tamaa"Dick aliongea kisha akafanya maombi ya kufunga mkutano ule ulioonekana kuwa mkubwa kuwahi kutokea Mjini KIGOMA!! ************** "Kweli maisha safari ndefu.........."Nasra aliongea wakati wapo ndani ya gari yao kwa ajili ya kurudi Dar es salaam "Mtu akisikiliza vizuri historia yenu anaweza akaona ni kama stori tu bila kujua ukweli halisi"Nasra alingea huku akitokwa machozi ya furaha "We acha tu mwanangu,,hakika hakuna binadamu anayepanga maisha yake bali kila anavyoishi mtu ni namna ya mipango ya MUNGU"Mama Ray aliongea huku akitokwa na machozi ya furaha pia "Yote niliyopitia ilikuwa ni lazima niishie huku,,ndo mana namshukuru Mungu kila kukicha kwa miujiza hii anayoendelea kunionyesha"Mama Ray aliongea huku Dick akiwa kimya akiendesha gari yake kwa umakini!! *********** Maisha ya wawili yale yalibadilika kabisa,,walizunguka Nchi nzima kwa ajili ya kutangaza neno la Mungu,,miaka miwili ikasiha hatimaye ukaja mwaka wa tatu Dick na Nasra wakafanikiwa kupata watoto mapacha wote wa kiume waliokuwa wakiitwa Martini na Marthias Maisha yakaendelea hatimaye ikaisha miaka minne mingine Nasra alifanikiwa tena kupata watoto mapacha wengine mmoja alikuwa wa kike na mmoja wa kiume wakawapa jina la Maria na Adam familia ilizidi kuwa kubwa!! Dick akaendelea kuzunguka kutangaza neno la Mungu akiwa na mama Ray,,hatimaye wakapata safari ya South Africa kwa ajili ya kuubiri Injili,,walifika mpaka South na kufanya kazi ya Mungu kwa muda wa siku kumi na nane "Kweli Mungu mkubwa mwanangu,,kwa kipato hiki tulichokipata lazima tukajenge kanisa letu tukifika Dar es salaam"Mama Ray almwambia Dick wakiwa ndani ya ndege wakirudi Tanzania "Ni wazo zuri lakini itapendeza zaidi kama tukitafuta eneo nje ya Dar es salaam"Dick aliongea huku akimuangalia mama Ray usoni,,mala ghafla ndege ikapoteza muelekeo,,abiria wote wakaombwa wafunge mikanda yao pamoja na madirisha kwani tayari ndege ilishamshinda rubani Vilio vilisikika watu wakililia familia zao,,Dick alifumba macho yake na kuanza kusali huku akiikabidhi familia yake kwa Mungu "Dick mwanangu,,tunakufa pamoja lakini naomba tusiitupe imani yetu"Mama Ray alimwambia Dick huku akimshika mkono!! Moja kwa moja ndege ilielekea kwenye mlima pembeni kabisa mwa bahari na kugonga mlima ule,,ndege iliripuka yote pamoja na abiria waliokuwemo na huo ndo ukawa mwisho wa maisha ya wawili wale!! "Duuuh Mchungaji Dickson kafa na #Sugar_Mamy wake"Baadhi ya watu waliokuwa wakifahamu historia ya wawil wale walisikika wakiongea,,ndugu waliombeleza kwa maombi na sala za kila aina na huo ndo ukawa mwisho wa Dick na #Sugar_Mamy!! M...W..I..S...H...O ************ Nawashukuru wote tuliokuwepo mwanzo hadi mwisho wa stori hii Pia nawashukuru wote ambao walikuwa wananiwezesha kwa namna moja au nyingine kufanikisha kutoka kwa stori kila siku Naamini mtakuwa mmejifunza mengi kupitia stori hii lakini kubwa zaidi ni kuhusu kujilinda dhid ya ukimwi!! By #HAJRAT
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 05:59:43 +0000

Trending Topics



>
★★★★★EARN $2,000-$8,000 PER MONTH WITHOUT EVER ENROLLING
Ok. Now in ticked off. You dont know me You stain. But i
[Xyne Engine] Audition AyoDance Hack 6104 / Jockey Service
ld that have to run
Biografía de Ricardo ArjonaRicardo Arjona nació el 19 de Enero

Recently Viewed Topics




© 2015