***********TAHADHARI********* EWE NDUGU YANGU TUJIFUNZE NA - TopicsExpress



          

***********TAHADHARI********* EWE NDUGU YANGU TUJIFUNZE NA TUELEWE KUWA UKWELI NI MIONGONI mwa sifa njema walizopambika nazo Mitume wa Mwenyezi Mungu. Qur-ani yatuambia:- NA MTAJE IDRIS KATIKA KITABU (hiki). BILA SHAKA YEYE ALIKUWA MKWELI SANA NA NABII. (19:56) Tabia ya ukweli huzaa matunda mema na mazuri ambayo huvunwa na watu wakweli. Miongoni mwa matunda hayo ni:- 1. Utulivu wa nafsi – Mwenye kupambika na tabia ya ukweli huwa na utulivu wa nafsi kwa mujibu wa kauli ya Mtume: Ukweli ni utulivu 2. Baraka katika chumo na ziada ya kheri – Bwana Mtume amesema: Wauzianaji(Muuzaji na mnunuzi) wana khiyari (ya kupitisha au kuvunja biashara) muda wa kuwa hawajatengana, wakiwa wakweli na wakabainisha (aibu za kinachouzwa) watabarikiwa katika biashara yao, na wakificha (aibu) na wakasema uongo itafutwa baraka ya biashara yao Al-bukhaariy 3. Kufuzu kwa kupata daraja ya mashahidi, hili linathibitishwa na kauli ya Mtume aliposema: Mtu atakayemuomba Mwenyezi Mungu kufa shahidi kwa ukweli, Mwenyezi Mungu atamfikisha daraja ya mashahidi hata akifia kitandani. Muslim 4. Kuepuka balaa, inasimuliwa kwamba mtu mmoja aliyekuwa anakimbizwa alikimbilia kwa mtu mwema mmoja akamuomba amfiche hasikamatwe. Yule mtu mwema akamwambia; Lala hapa, akamfunika na rundo la makuti. Wale waliokuwa wanamkimbiza wakapita pale kwa yule mtu mwema wakamuuliza :Umemuona mtu akipita hapa anakimbia? Akawajibu: Huyo hapo chini ya makuti. Wale watu wakamuona nawafanyia maskhara wakampuuza wakaenda zao. Yule mtu aliyekuwa akikimbizwa akaokoka kwa bababu ya ukweli wa mtu mwema yule. 5. Kuchuma mapenzi ya Mola na watu. Mtu mkweli hupendeza mbele ya Mwenyezi Mungu na watu na watu wema humpenda. EWE NDUGU YANGU TUSOME KWA MAKINI KWANI YAPO MAZINGATIO MAKUBWA In shaa ALLAH tulale salama ndugu zangu
Posted on: Fri, 08 Nov 2013 18:31:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015