THE AFRICAN BEAUTY Zawadi na mama yake wanaishi uswahilini katika - TopicsExpress



          

THE AFRICAN BEAUTY Zawadi na mama yake wanaishi uswahilini katika nchi ya kenya wanaishi wawili tu, miaka miwili miaka mitano iliyopita walikimbiwa na baba mzazi wa zawadi kwa ajili ya kukwepa gharama za matibabu ya ugonjwa wa moyo anaoumwa zawadi. zawadi anaumwa amepakatwa na mama yake nje ya nyumba yao kwenye mkeka akiwa na umri wa miaka 10 ana muuliza mama yake. ZAWADI Mama ulisema nikifikisha miaka 15 utanifanyia birthday utanipa zawadi gani?. MAMA Bado muda haujafika lakini nakuahidi nitakuandalia zawadi nzuriiiii. Miaka 5 baadae. Wapo ndani ya nyumba pamoja na majirani kwenye happy birthday ya zawadi. Sherehe inaendelea wakati wa mama mzazi kutoa zawadi.mama anaangalia bangili na hereni za mbao alizo nunua sokoni kwa uchungu anakata shauri na kukunja mfuko uliohifadhia . mara ghafla zawadi anaanguka na kukimbizwa hospital. Madaktari wakamchunguza na kusema tatizo lake lilikuwa ni moyo na kwa vyoyote vile kwa jinsi moyo wake ulivyo angeaga dunia.mama yupo pembeni ya kitanda cha zawadi ZAWADI(anatirikwa na machozi) mama nimesikia kuwa madaktari wanakwambia kuwa nitakufa? MAMA (anamfuta machozi) hutakufa utaishi mwanangu. ZAWADI Una uhakika gani mama?. mama machozi yanamlenga anashindwa kuvumila kumface zawadi anageukia pembeni na kuinuka MAMA Bado mdogo sana kukabili kifo.hutokufa kwa sababu ya upendo . mama hakuhuzuria tena hospitalini wiki moja baadae.zawadi alifanyiwa opereshen pasipo kuonana na mama yake.alipopata nafuu alimuuliza docter aliyemfanyia opereshen ZAWADI Docter simwoni mama yangu niambieni kama na yeye amenitelekeza DOCTER hapana mama yako huwa anakuja mara kwa mara ila anashindwa kukuona kwa ajili ya uchungu alio nao ukipona utaonana nae yeye anafanya kazi ya kutafuta hela ya chakula na matibabu yako Siku ya kutolewa hospitali docter aliye mfanyia opereshenon anaongozana nae hadi nyumbani kwao anakuta majirani wanampokea kwa furaha na kumkaribisha muda mchache anaulizia mama yake DOCTER Nilishindwa kukuambia ila mama yako ameacha zawadi yako yenye maelezo yote Majirani wanaleta box lililoandkwa happy birthday zawadi.anafungua ndani kuna mfuko una zawadi ya bangili na hereni za mbao zawadi anatabasam pembeni kuna barua anaikunjua na kuisoma sura ya furaha inabadilika na kuwa majonzi BARUA Mwanangu mpendwa natumaini unaendelea vizuri hadi unaposoma barua hii, siku uliponiuliza nitakupa zawadi gani ya siku yako ya kuzaliwa sikujua ni zawadi gani ningekupa wewe. zawadi ya hereni na bangili sikuona ni vya samani kwako, lakini kwa hali uliyonayo ilinibidi nikupe moyo wangu wangu wa upendo ili uendelee kuishi siwezi kukutelekeza siku zote nitaishi pembeni ya ubavu wako naimani utaishi wa ajili ya upendo nilio nao kako♥♥♥♥♥♥♥♥♥♥♥♥♥♥ Zawadi anamaliza kusoma barua imelowa machozi anamgeukia dactari taratibu anamsogelea mdomo wake ukitetemeka anashindwa kuongea anampiga daktari ngumi za kifuani ZAWADI Kwanini, kwanini mama yanguuu…. Anashindwa kuendelea kuongea nguvu zinamwishia dactari ana mdaka na kumkumbatia… THAT WAS A BEGINNING OF THE STORY OF THE AFRICAN BEAUTY……………..
Posted on: Sun, 08 Sep 2013 14:33:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015