Tangazo la ajira jeshi la polisi 2014/2015 Ajira kwa - TopicsExpress



          

Tangazo la ajira jeshi la polisi 2014/2015 Ajira kwa Wahitimu Elimu ya Juu Mwaka 2014 Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo. Inspekta Jeneraliwa Polisi, Makao Makuu ya Polisi, S.L.P.9141, DARESSALAAM Waombaji wawe na taaluma zifuatazo: Shahada:Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi waUmma,Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi,Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji [BaLE],Sheria,Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa Habari, Uandishi wa Habari za Michezo,Mawasiliano ya Umma,TV&Redio Production,Michezo, Ugavi[BAinProcurement &Supplies], Mawasiliano ya Redio [BscinRadio Communication], Mazingira[BAin Environmental Disaster Mgt],Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering],Uchoraji [BAinFineArts], Fedha na Benki[Finance &Banking],Daktari [MedicalDoctor]na Daktari wa Meno[Dental Surgeon],Mkemia, Bailojia[Molecular Biology]. Stashahada:Utunzaji Kumbukumbu,Katibu Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya Redio, Matengenezo ya Kompyuta,Fax na Photocopy Machines, Mafundi Mitambo wa Meli,Mafundi Umeme wa Magari,Ugavi [Procurement& Supplies],TVnaVideo Production,Manahodha, Tabibu[Clinical Officer],Tabibu wa Meno[DentalTherapist], Mzoezi ya Viungo [Psysiotherapist/ Occupational Therapist],Fundi Sanifu Mionzi [Radiographer]naFundi Sanifu Macho [Optometrist]. Astashahada: Uzamiaji, Mpishi,Fundi Pikipiki, Fundi Ushonaji na Muuguzi Msaidizi [EnrolledNurse]. MASHARTI KWA MWOMBAJI 1.Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika picha yake“PptSize” kwenye fomu. 2.Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote yaani cheti cha kuzaliwa,kuhitimu elimu ya sekondari [Leaving &Academic],cheti/ vyeti vya taaluma [AcademicTranscript]. 3.Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. SIFA ZA MWOMBAJI 1.Awe Mtanzania kwa kuzaliwa. 2.Awe na umri usiopungua miaka18 na usiozidi miaka25. 3.Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu. 4.Awe natabia njema. 5.Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu. 6.Awe na afya njema [kimwili na kiakili] 7.Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto. 8.Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu]. 9.Awe na urefu usiopungua sentimita 155. 10.Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya. 11.Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini. 12.Awetayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi. 13.Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje . fomu ya ajira elimu ya juu (1).pdf
Posted on: Tue, 05 Aug 2014 13:54:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015