UJINGA-BUSARA Mlimuona Rais Obama? Mliiona bendera ya nchi - TopicsExpress



          

UJINGA-BUSARA Mlimuona Rais Obama? Mliiona bendera ya nchi yake? Mliiona BENDERA YA CHAMA CHAKE? Mlimsikia akizungumzia kuhusu chama chake? Naziona za CCM zikipepea huku japo hata ya chama cha hapa siijui. Nawasikia viongozi wetu wakitumbukiza u-chama hata katika ziara za kitaifa. KWANINI HATUJIFUNZI MEMA TOKA KWA HAWA WAGENI WETU? SERIKALI na viongozi wetu wanaamua NINI WAJIFUNZE KUTOKA KWAO (kwa kuwa wanachochagua kinawanufaisha) Nilishatoa mfano..... Ukizungumzia Demokrasia na miundombinu ya Marekani, viongozi wetu watakwambia "hao wamekuwa huru zaidi ya miaka 300 ilhali sisi hata 60 hatujafika" SAWA... Tuangalie MATUMIZI basiiiiii Mbona hamtumii magari waliyokuwa wakitumia walipokuwa na miaka 60 ya Uhuru? Mbona hamlipwi mshahara waliokuwa wakiupata walipokuwa na miaka 60 ya Uhuru? Kuna MENGI YA MAANA YA KUJIFUNZA kwenye ziara hizi zaidi ya HOTUBA, MAGARI, NDEGE, USALAMA nk Viongozi na wananchi tujifunze kuwajibika. Viongozi na wananchi tujifunze kuwajibishana. Nawaza kwa sauti tuuuuuuuu !!!!!!!!!!!!!!!!!!
Posted on: Wed, 03 Jul 2013 09:25:29 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015