Waandamanaji wapambana na polisi Misri Polisi wa kuzuia ghasia - TopicsExpress



          

Waandamanaji wapambana na polisi Misri Polisi wa kuzuia ghasia nchini Misri wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji, na wameufunga uwanja wa Tahrir na mitaa muhimu ya Cairo, baada ya kutokea makabiliano baina ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa, Mohamed Mursi, na wale wanaompinga. Wanajeshi wametumia vifaru na senyenge kuziba njia za kuingia katika uwanja huo, na kuyalazimisha magari yatokayo katikati mwa mji kubadilisha njia, wakati maelfu ya wafuasi wa Mursi kutoka wilaya mbali mbali za Cairo walipokuwa wakijaribu kukutana katika uwanja wa Tahrir. Polisi pia walifyatua risasi hewani na kutumia gesi ya kutoa machozi katika maeneo mengine ya mji, ambako waandamanaji walikuwa wakirushiana mawe.
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 07:09:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015