Wakaaji wa eneo la kibiashara; Saligaa Nakuru, tumeamshwa - TopicsExpress



          

Wakaaji wa eneo la kibiashara; Saligaa Nakuru, tumeamshwa usingizini na visa viwili tofauti vya kutamausha, Kisa cha kwanza: Jamaa wa umri wa makamu amepatikana amefariki kando mwa barabara baada ya kugongwa na gari isiyojulikana. Maiti ingali katika eneo la ajali ikisubiri Polisi ndiposa iweze kutambulika. Kisa cha Pili: Papo hapo moto mkubwa umeweza kuteketeza mali ya thamana isiyojulikana katika nyumba za kukondisha. Wapangaji wamelazimika kukaa kwa baridi huku wakikadilia hasara ya moto huo. Yaaminika hakuna aliyepoteza maisha. Chanzo cha moto huo hakijabainika
Posted on: Thu, 18 Jul 2013 01:52:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015