[email protected] 02.07.013 CORD Muungano wa cord umejiunga na - TopicsExpress



          

[email protected] 02.07.013 CORD Muungano wa cord umejiunga na shirikisho la watumizi wa bidhaa nchini KOFFEC katika kupinga kuidhinishwa kwa mswada kuhusu utozaji ushuru kwenye bidhaa muhimu na unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni hii leo. Kupitia katibu wa muungano huo Professa Anyan’g Nyong’o wanasema kuwa iwapo utapitishwa basi utaathiri pakubwa maisha ya mwananchi wa kawaida. Mswada huo ambao utaanza kujadiliwa katika bunge la kitaifa hii leo unapendekeza asilimia 16 kwenye ushuru wa bidhaa muhimu za nyumbani. WALIMU Huenda walimu wa shule za umma kote nchini wakafutwa kazi na kukosa marupurupu yao ikiwa serikali itatekeleza maamuzi ya mahakama ya viwanda ya kuwataka walimu warudi kazini mara moja au wachukuliwe hatua za kisheria. Haya ni kwa mujibu wa wakili Yusuf Abubakar ambaye amesema kwa sasa walimu wana njia moja tu ya kuwasaidia kufikia malengo yao nayo ni kukata rufaa ili mahakama isitishe uwamuzi uliotolewa hapo jana ama waitake mahakama isikize kesi hiyo upya kwa sababu hawajaridhika na uwamuzi uliotolewa. Yusuf ameongeza kwamba iwapo walimu bado wanategemea mkataba uliotiwa sahihi baina yao na serikali mwaka 1997 basi hawana tena nafasi kwa sababu kulingana na katiba mpya kuna tume ya mishahara ambayo inasimamia maswala ya mishahara kwa wafanyikazi. WAKUU Huku hayo yakijiri tume ya TSC imewaamuru wakuu wa shule mbalimbali kuendesha uchunguzi katika shule zao kubaini idadi ya walimu waliotii agizo la mahakama na kuregea shuleni. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama hicho Wilson Sossion bado hawajapokea agizo rasmi la mahakama Haya yanajiri baada ya agizo kutolewa na mahakama ya viwanda ya kuwataka walimu kuregea shuleni au hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. MAKUENI Kampeni za kujipigia debe kwa wadhifa wa useneta katika kaunti ya Makueni zimeendelea kushika kasi huku mgombea wa wadhifa huo kwa tiketi ya muungano wa CORD Kethi Kilonzo akitarajiwa kuelekeza kampeni zake katika eneo la Kilowi akiandamana na viongozi wa mrengo huo. Aidha wapiga kura wawili wanatarajiwa kufika mbele ya tume ya uchaguzi na mipaka kutoa kile wanachokitaja kama ushahidi kudhibitisha kuwa Kethi Kilonzo hajajisajili kama mpiga kura Mombasa Serikali ya kaunti ya Mombasa inatarajiwa kuzindua sheria mpya za trafiki hii leo ili kukabiliana na msongamano wa magari. Gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho anatarajiwa kuzindua sheria hizo mpya za barabarani zitakazokabiliana na msongamano katika barabara za kaunti hiyo. Shughuli hiyo itafanyika katika mzunguko wa changamwe ambapo sheria hizo zinatazamiwa kuwa mwanzo mwema wa kuondoa msongamano unaoendelea kushuhudiwa kila uchao hasa nyakati za asubuhi na jioni. KIMATAIFA Marekani Rais wa marekani aliye ziarani Barani Afrika Barrack Obama amemtaka rais wa Misri Mohammed Mursi kutafuta suluhu la haraka kwa machafuko yanayoshuhudiwa nchini humo na ambayo yamepelekea kuuwawa kwa watu wanne na wengine wengi kujeruhiwa. Kwa mujibu wa ujumbe kutoka ikulu ya Marekani Obama aliwasiliana na rais Mursi akiwa nchini Tanzania na kusema kuwa marekani imejitolea kuhakikisha kuwa kuna demokrasia nchini humo na kushikilia kuwa marekani haiegemei upande wowote.
Posted on: Tue, 02 Jul 2013 09:24:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015