"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba - TopicsExpress



          

"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba xxxvii "Pumbavuuu............"Nilimsikia jamaa mmoja akiongea huku akiingia ndani "Yani unatembea na mwanafunzi alafu unatuuliza eti tunasemaje....."Jamaa yule aliongea huku akionekana dhahiri kukasirika "Kwani we nani bro.......?"Nilijikuta nikimuuliza yule jamaa kwa sauti ya upole "Mda si mrefu utanijua mi ni nani......!!"Jamaa yule aliongea huku akimuangalia Anitha aliyekuwa amejifunika na shuka "Ndo nyie nyie mnaowaharibu watoto wa kike nchini"Jamaa yule aliendelea kufoka huku wale wenzake wakiwa kimya wakimsikiliza Kijasho chembamba kilianza kunitoka mtoto wa kiume,,nilimuona Anitha naye akitetemeka nikajua fika nilikuwa nimekwisha "Bro si tuyamalize wenyewe achana na kupiga simu"Nilimwambia yule jamaa baada ya kumuona anahangaika na kupiga simu "Ngoja nivaege ili ata kama polisi wakitokea wanikute na nguo"Niliwaza huku nikianza kuvaa viwalo vyangu kimoja badala ya kingine "Na we leo utatueleza,,yani kusoma husomi sababu ya huyu mpuuzi wako si ndio enheee...."Jamaa yule alimwambia Anitha kwa hasira!! "Hallow..........."Jamaa nilimsikia akiongea "Aaah simu yangu imeisha hela....."Jamaa alilalamika huku akiingiza mkono kwenye mfuko wa suruali yake kisha akatoa noti ya shilingi elfu mbili akampa mmoja kati ya wale vijana aliokuja nao "Kaniletee tigo ya elfu mbili"Jamaa yule alitoa maagizo huku akiniangalia kwa jicho lililoonyesha chuki dhidi yangu haraka nikajua kama ningezubaa basi uhai wangu ungekuwa shakani siku ile "Mama Salma anawatafuta sana watu kama nyie"Jamaa aliongea huku akizunguka huku na kule "Lakini..............."Nilijaribu kutaka kuongea "Hakuna cha lakini lazima nitahakikisha unakwenda jela"Jamaa aliongea kwa hasira,,sikutaka tena kushangaa kwani nilielewa fika kauli mbiu ya mke wa Jakaya "Hapana sipo tayari kwenda jela kwa miaka thelathini"Niliwaza huku nikiangali kushoto na kulia!! Kama mshale au risasi,,yani ni zaidi ya rocket kwa jinsi nilivyochomok katikati ya wale jamaa waliokuwa wamesimama mlangoni "Mwiziiii huyooooooooo......."Jamaa niliwasikia wakiita lakini sikutamani kusimama,,nikazidi kuongeza mwendo wa kukimbia nikielekea lilipokuwa geti la kutokea nje ya Lodge ile Nilipokaribia getini nilimuona mdada mmoja akiingia ndani ya ile Lodge "We dada pisha hapo getini........"Niliongea kwa sauti kwani sikutaka kumkumba dada yule asiyekuwa na hatia Kwa spidi niliyokuwa nayo niliwaacha mbali waliokuwa wakinikimbiza kwani hadi nafika nje ya geti sikusikia tena nikiitiwa mwizi wala sikuwaona waliokuwa wakinikimbiza mana muda wote nilikuwa nikigeuka nyuma!! *********** Kwakweli siwezi kuwaambieni nilipita njia gani na nilitumia mda gani kufika nyumbani ila ninachokikumbuka nilifika nyumbani nikamkuta mama amesimama mlangoni "Una nini we mtoto........?"Mama aliniuliza huku akinishangaa "Funga mlango mama,,funga mlango wasiingie"Niliongea kama mtu niliyechanganyikiwa "Wakina nani...........?"Mama aliniuliza "Polisi,,polisi wanataka kunikamata"Nilimwambia mama huku nikihema kwa nguvu "Kwa kosa gani mwanangu......?"Mama aliniuliza huku akiniangalia kwa macho ya huruma "Mama nimekutwa na............"Nilisita kumueleza mama ukweli "Na nini...........?"Mama aliendelea kuniuliza "Ngo ngo ngo"Mlango wetu tuliusikia ukigongwa kwa nguvu "Karibu............."Mama aliitikia huku akianza kutembea kwenda kuufungua haraka nikamshika mkono "Mama usiende kuufungua mlango nakuomba"Nilimwambia mama huku nikikaa mbele yake kumzuia asiende kuufungua mlango "Ngo ngo ngo ngo......."Mlango ulisikika tena na safari hii ilikuwa kwa nguvu zaidi ya mwanzo "Nakuja..........."Mama aliitikia na kunisukumiza pembeni kisha akaendelea na safari yake ya kuelekea mlangoni nikajua tayari nilishakwisha!! Mama alipoufungua mlango wakaingia watu wanne,,askari wawili,,bosi wangu pamoja na Magreth "Mungu wangu............"Niliongea huku nikimuangalia Magreth usoni "Wilbat una nini lakini........?"Magreth aliniuliza huku akitokwa na machozi na kwamala ya kwanza nilianza kujiona Lofa tena wa mwisho kabisa "Kumbe aliyokuwa akiyasema #Mchopa ni ya kweli kabisa"Niliwaza huku nikimuangalia polisi aliyekuwa anakuja nilipo na pingu mkononi "Enheee Magreth,,Wilibat amefanyaje tena........?"Mama alimuuliza Magreth huku akiniangalia mimi usoni "Kijana nadhani unayakumbuka vyema masharti tuliyokuwa tumekupa wakati unaanza kazi"Bosi aliniambia wakati askari mmoja ananifunga pingu "Tutakapoipata gari yetu na baadhi ya mambo mengine ya kiofisi basi tutakuachia huru"Bosi aliongea huku akigeuza na kutoka nje wakaniacha mi nikipandishwa kwenye difenda ya polisi kwa ajili ya kupelekwa kituoni!! ************ Usikose Kusoma Sehemu Inayofuata Nawashukuru Sana Watu Wanaoendelea Kunisapoti Kwa Kutuma Pesa Zao Kwa Ajili Ya Kusoma Stori Zangu Na Wewe Ambaye Bado Hujatuma Pesa Pia Nakushukuru Kwani Ata Comment Na Like Zako Ni Mchango Tosha Kwangu Unaosababisha Niendelee Kuimarika Day After Day Usiku Mwema By #Hajrat
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 20:45:01 +0000

Trending Topics



at us & say that house
Pastor Gerry Stoltzfoos is in the ICU. We just spoke to the

Recently Viewed Topics




© 2015