ZINGATIA EWE MUISLAMU Mmoja wa watu wema anasema Ninapomuomba - TopicsExpress



          

ZINGATIA EWE MUISLAMU Mmoja wa watu wema anasema Ninapomuomba Allah kitu akinipa nafurahi mara moja na ninapomuomba Allah kitu asiponipa basi nafurahi mara kumi.Akaulizwa kwa nini huwa hivyo?Akasema nilichoomba nikapewa hilo ni chaguo langu na nilichoomba nisipewe hilo ni chaguo la Allah kwani hakika Allah ni mwenye kujua ghaib na mwenye kujua lipi ni bora zaidi kwangu mimi na ninajua Allah atanipa lilo bora zaidi ya lile niloliomba.” Ni maneno yenye hekima yanahitaji mazingatio kwa kila muislamu.Sio kila unachoomba kina kheri na wewe.Vyengine havina kheri na wewe na Allah anakuepusha navyo hivyo ni wajibu wako kumshukuru Allah na kufurahi kwa kuwa amekulinda nacho na pale anapokupa basi pia ni wajibu ufurahi Allah kukupa kile ulichokiomba.Na pia tutumie silaha yetu ya kila jambo kumuomba Allah katika dua zetu kwani kwa hakika Allah atatujibu tu dua zetu.Allah anasema” Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni.(40:60)”.Na Mtume(swalla Allahu alayhi wasallam) anasema “Dua ndio uti wa mgogo katika ibada” Ewe mwenye huzuni,ewe mwenye matatizo ewe mwenye jambo lolote muelekee Allah na muombe juu ya jambo hilo.Tusisahau kuwaombea dua wazee wetu nao walotangulia mbele ya haki Allah awarehemu mwenye huzuni Allah amuondoshee huzuni mwenye maradhi Allah ampe shifaa ya maradhi yake na mwenye uzito katika mambo yake Allah ampe wepesi.Aaamin.
Posted on: Sat, 23 Nov 2013 21:35:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015