Zamani ukiwa na noti chakavu, ukipeleka benki unabadilishiwa mara - TopicsExpress



          

Zamani ukiwa na noti chakavu, ukipeleka benki unabadilishiwa mara moja. Ukiwa na kipande halali kama cha noti ya shilingi 10 (siyo elfu 10 bali 10) ukipeleka benki unapewa noti ya shilingi tano, yaani nusu yake. Mantiki ni kwamba kuna siku mahali fulani mtu atapeleka kipande kile cha pili na akipewa shiling tano ina maana noti nzima itakuwa imelipiwa shilingi 10. Sasa hivi benki hawapokei noti mbovu hata iliyowekewa gundi gundi tu za nailoni lakini yenye kila uhalali! Kibaya zaidi kuna rafiki yangu alitoa noti kwenye ATM ya benki fulani, alipoingia ndani kuomba kubadilishiwa,kukawa na kimbembe, jamaa wamekomaa na kumtaka aoneshe ushahidi. Alionesha risiti akabadilishiwa kwa shingo upande(msiwe mnazichana risiti mpaka mhakikishe hakuna tatizo na noti mnazotoa ATM). Wimbi la kugomea noti mbovu, hata zenye kila uhalali,limekuwa kubwa mno miongoni mwa watanzania, wasiwasi ukiwa nikiikubali, nitaipeleka wapi wakati benki zenyewe hazizitaki? Matokeo yake kuna noti nyingi za shilingi mia tano, elfu moja, elfu mbili, tano na 10 zimetoka kwenye mzunguko wa fedha na hili ni jambo endelevu kwani kila siku zinatokea noti za kukataliwa. Wachumi wetu waliangalie hili kwani kama kila siku Tanzania shilingi milioni moja inatoka kwenye mzunguko, ina maana kwa mwezi mmoja milioni 30 na mwaka milioni 360, miaka mitatu tu over one billion nje ya mzunguko! Ni vizuri itengenezwe sera madhubuti,yauhakika dhidi ya noti zinazochakaa, ni zipi zisiogopewe na vipi mmoja akiwa nayo akinunua kwa mwingine awe na uhakika wa noti hiyo kutomsumbua yeye kwani kwa sasa ukibambikiwa nayo,hiyo yako hiyo mpaka itakapotoka kwenye mzunguko kwani hakuna atakayekubali kuhangaika nayo, hata benki haikubali! Sera hiyo itengenezwe ili fedha yetu isipungue kwenye mzunguko kwa njia hii kuathiri uchumi wetu. Usijali sana takwimu zangu, hizo nimezitaja tu. Ikiwezekana serikali kupitia wizara ya fedha itangaze operesheni ya mwezi mmoja tu kukusanya noti zote zilizoko majumbani Tanzania nzima zilizoondolewa kwenye mzunguko kwa uchakavu ili zirudishwe kwenye mzunguko. Nawasilisha.
Posted on: Thu, 10 Oct 2013 05:47:29 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015