2nd Septemba 2013 Mukhtasari wa habari @ 1pm Rais Uhuru kenyatta - TopicsExpress



          

2nd Septemba 2013 Mukhtasari wa habari @ 1pm Rais Uhuru kenyatta ametoa hati miliki alfu kumi na nne mia tatu na themanini na moja kwa wakaazi wa Kwale Rais ametawazwa kuwa mzee wa kaya mijikenda. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Mikakati ya mipango ya afya kwa kipindi cha miaka mitano katika kaunti ya Mombasa imezinduliwa rasmi na gavana Ali Hassan Joho. ,,,,,,,,,,,,,,, Aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya utoaji wa liseni kwa magari ya umma Hassan Ole Kamwaro amepinga vikali hatua ya kupiga marufuku magari ya kubeba abiria kuhudumu wakati wa usiku. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Inspekta generali wa polisi David Kimaiyo amewataka viongozi wote wa kisiasa kutoka kaunti ya Marsabit kuandika taarifa katika idara ya upelelezi CID kufuatia ghasia zilizokuwa zikiendelea katika kaunti hiyo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Taarifa kutoka mjini Damascus imesema kuwa hatua yoyote ya kijeshi itakayochukuliwa na nchi ya Marekani dhidi ya Syria huenda ikachochea usaidizi kwa wapiganaji wa Al- Qaeda. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Posted on: Mon, 02 Sep 2013 10:04:41 +0000

Trending Topics



div>

Recently Viewed Topics




© 2015