CALVIN AND ALVIN (LOVE STORY) SEHEMU YA 14 Mimi na Alvin tulikua - TopicsExpress



          

CALVIN AND ALVIN (LOVE STORY) SEHEMU YA 14 Mimi na Alvin tulikua tumeenda Makaburini kufagilia kaburi la baba yetu kwasababu kesho yake ndo ilikua arobaini yam zee Ambonile toka afariki dunia, tukiwa makabirini hapo huku tumevalia nguo nyeusi na miwani nyeusi ilikuja gari aina ya Toyota Surf na wakateremka vijana wawili ambao walikua warefu, walikuja mpaka pale tulipokua mimi na Alvin kisha mmoja wao akasema “mambo Alvin” Alvin aliitikia salamu kisha wakanigeukia mimi na kuniambia samahani japo tunafahamu wewe ni mwanasheria mkubwa sana mimi ni police mpelelezi naitwa James na huyu anaitwa Massud huku wakitoa vitambulisho vyao vya upolisi na kummwambia Alvin upo chini ya Ulinzi huku wakimuomba mikono wamfunge pingu “hey nimefanya nini tena?” “utajua huko huko police” “noo hamnipereki bila kuniambia kosa” “Alvin nenda usibishane nayo nipo kukusaidia” nilimwambia Alvin wakamchukua na kuondokanae huku wakiniambia kituo cha polisi ambacho wanampereka Baada ya wao kuondoka mie niliondoka pale makaburini na kuelekea nyumbani kumpa mama taarifa juu ya yote ambayo yamempata Alvin, kwakua mama alikua ananiamini sana kwa kazi yangu ya uanasheria hivyo hakuwa na wasiwasi juu ya hilo aliamini muda mchache tu Alvin atarudi nyumbani… *************** Niliondoka na kwenda kufuatilia kosa ambalo Alvin alikua amefanya ndipo nilipokutana na majanga kituoni hapo…Alvin alikua na kesi ya kumtorosha mwanafunzi shule na kuishinae nyumbani kwake kama mke wake kwa muda wa miezi mitatu mototo haonekani nyumbani wala shuleni, Alvin anakesi ya kumpa mamba mwanafunzi huyo huyo ambaye alimtoa shule na kumfungia nyumbani kwake, Alvin amepewa kesi ya kumuharibia mwanafunzi masomo yake na kupoteza Ada za wazazi ambazo walikua wanamlipia huyo mwanafunzi…. Niliishiwa nguvu kabisa na nilishindwa nianzie wapi kumtetea Alvin kutokana na kesi yake jinsi ilivyo kwasababu ni wazi kabisa inaonyesha hatutaweza kushinda kutokana na sheria ambazo zimewekwa na rais wetu juu ya wanafunzi… Ilinibidi niombe kukutana na huyo Mwanafunzi na wazazi wake ili tupate kuongea machache ambayo yanaweza kuwasaidia wao na sisi pia, hapo ndipo aibu iliponijaa usoni Mzazi wa huyo mwanamke ni Mzee Mwaipoje ambaye nilishawahi kumshinda kwenye kesi yake moja hivi ambayo nilipewa nisimamie na tukamshinda yule mzee japo alitumia pesa nyingi sana pia alidiriki kunipa rushwa ili niiachie ile kesi aiendeshe wakili mwingine ila nilimkatalia, hapo ndipo nikaona mdogo wangu Alvin anaenda kuozea jela… Muda mchache tukiwa kituoni hapo kwenye chumba cha upelelezi polisi mmoja alitumwa na mkuu wa upelelezi aletwe huyo mwanafunzi ndipo alipoingia binti ambaye sikuamini macho yangu, Alikua ni prisca huku ameshikilia tumbo lake na mkono wa kushoto anatafuna karoti… Niliona aibu nikainama chini bila kusema chochote, mikono ilitetemeka huku jasho likinitoka kwenye vidole vya mikono yangu, niliinua uso na kumuangalia prisca usoni lakini Prisca alionekana kama mtu asiye na wasiwasi wowote ule huku akiendelea kutafuna ile karoti kama mtu mwenye njaa kali sana “kijana unataka uzungumze nini na mimi?”aliniuliza baba yake Prisca Nilikosa chakuongea kwasababu yule binti namfahamu na nilikua najua wazi kabisa anamahusiano na Alvin ila nilikua sijui kama ni mwanafunzi kama maelezo yalivyoandikwa kwenye file ambalo amefunguliwa kesi Alvin “ulikua unasoma form ngapi?” nilikua nimemgeukia Prisca na kumuuliza “Nilikua form Five mwenzio” alijibu huku akisuguasugua miguu chini huku mkono mmoja akiwa bado anatafuna karoti huku akiendelea kupapasapapasa tumbo lake ambalo juu yake alikua amevalia tshert iliyokua imeandikwa “FOOT PRINT” “afande hebu ona huyo mwanamke maandishi yaliyoandikwa kwenye Tshert yake, eti FOOT PRINT, wameshakuprint hilo tumbo tayari” Alisema afande mmoja hivi wakike ambaye alikua amekaa pembeni ya Prisca… “wee unamfahamu huyu?” Aliuliza mmoja wa polisi “ndio namfahamu kaka yake na Alvin..” Alisema Prisca Tuliongea mengi sana lakini hakuna hata moja tuiloelewana na mwisho wa siku tuliamua tu kesi ifikishwe mahakamani kutokana na kutofika muafaka SIKU YA KESI Wakili ambaye alikua anasimamia ile kesi ni Rolyn mwanamke ambaye nilikua nampenda sana muda mrefu, nilishawahi kujaribu kufanya mipango mingi ili nikahakishe nitampaje nilishindwa, huyu Rolyn nilishawahi kuwa naye Ofisi moja ya Mawakili wa kujitegemea na alishawahi kunishtaki kwa bosi wangu kwamba namsumbua sana pale ofisini na huyo bosi akaamua kuniita na kunionya juu ya hilo suala, Kwakua nilikua na True feelings of love nilijikuta nashindwa kuvumilia juu ya upendo niliokua nao kwa huyo Rolyn ambaye aliletwa ofisini hapo ili kuongeza nguvu ya kuwa na mawakili ambao wachapa kazi hodari…. Niliendelea kumsumbua Rolyn kwamba nahitaji kumuoa lakini haikuwa hivyo kama nilivyotegemea mwisho wa siku nilisimamishwa kazi kwa muda wa mwezi mzima ndipo nikaona nisirudi tena pale ofisini na kupata Ofisi nyingine ambayo naifanyia kazi mpaka sasa, kiukweli nilimpenda Rolyn na bado ananafasi kubwa ndani ya moyo wangu, ni mwanamke ambaye ameiweza akili yangu na kunifanya nianze kumpenda zaidi ya vile mwanzo…. (ni short story kuhusu Rolyn) Sheria inasema mwanasheria wa upande mmoja (mshtaki) akihisi anahisia za kimapenzi na mwanasheria wa upande wa pili(mtuhumiwa) anaruhusiwa kuhailisha kesi na akatafuta wakili mwingi, hivyo ndo ilivyokua kwaupande wangu kwamba nilikua nampenda Rolyn zaidi ya maelezo, na kuna muda Alvin aliniita na kuninong`oneza “kaka huyo wakili si ndo yule aliyekusababishia uachishwe kazi pale WAKILI KWANZA?” “Yap ndo yeye umemkumbuka eeh?” “ndio kaka, sasa unauhakika tutamshinda kweli maana uliniambia yupo fit na anaijua sana sheria” “usijali Alvin kesi tutashinda” nilimjibu Alvin kisha nikarudi kuketi nilipokuanimekaa Alvin alikua pale kizimbani upande wa kushoto wakati huo upande wa kulia alipanda Prisca huku akiwa anakula karoti kama kawaida yake na mkono mwingine akiwa ameshika kopo dogo la chupo ya uhai kwaajili ya kutemea mate…ITAENDELEA
Posted on: Thu, 29 Aug 2013 08:04:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015