Hivi kwanini tunalipia Gharama za kuvuta Umeme...?? Mi nadhani ni - TopicsExpress



          

Hivi kwanini tunalipia Gharama za kuvuta Umeme...?? Mi nadhani ni kama vile kuweka kiingilio Dukani... Ukitaka kuja kununua nguo say kwenye duka fulani ulipe kiingilio mlangoni halaf ndio ukachague unachotaka na ukipata bidhaa Ulipie Tena... Sisi ni wateja wa Tanesco, tunapochargiwa connection fee na nguzo fee, wakati hatuelezwi hizo fedha zinarudije kwa mteja ni utemi flani....Kwasababu siku ukitaka kuachana na Tanesco ukawaambia wakupe Nguzo zako ulizonunua, Ukachane hata mbao za kujengea banda la kuku, Je watakupa? Na kama sababu ni kwamba wengine watakuwa wanatumia nguzo hizo hizo kupata umeme, kwanini wasikurefund pesa zako basi, hata kwa depreciation... Tunalipa Gharama kuubwa kwa umeme wa mashaka... Mara umekuja mwingi unaunguza vitu na nyumba za watu, mara umekuja mdogo hauwezi kuwasha pasi... Mara ohooo Mgao miezi sita kwa masaa 16 nchi nzima... Wananchi tusikubali kuburuzwa namna hii..Kwakuwa system ni corrupt...Basi, Ni wakati Muafaka Kuanza kutumia Umeme Jua au njia nyingine za kuzalisha umeme kama upepo nk...halafu tuone na hizo wanatucharge connection fee, au solar panels ownership fee... Kwa mtu anayehitajika kuvuta umeme kwa kutumia nguzo tatu au nne, anaweza kabisa kuafford kuwa na umeme wake mwenyewe unaotumia Solar, tena bila hata ya gharama za uendeshaji na matumizi kama vile Luku.... NI MTAZAMO TU.
Posted on: Wed, 13 Nov 2013 13:53:54 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015