Jiunge nami Maryam Dodo Abdalla katika Amka na BBC leo - TopicsExpress



          

Jiunge nami Maryam Dodo Abdalla katika Amka na BBC leo ambapo: Katibu mkuu wa Umoja mataifa Ban Ki Moon ameunga mkono kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya kati katika kuzuia machafuko yanayoendelea. Na leo tuko Daadab, Kaskazini mashariki mwa Kenya. Tunaangalia vipi makubaliano ya kuwataka wakimbizi wa Somalia warudi nyumbani kwa hiari, yanavyopokewa. Na washika dau katika sekta ya uchumi na maendeleo wanakutana leo huko Kuwait kuimarisha biashara kati ya nchi za Kiafrika na za Kiarabu. Je huu ndio mwanzo wa mwisho wa nafasi ya mataifa ya magharibi katika uchumi wa Afrika? Karibu!
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 02:35:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015