KWA MUKTASA YALIYOJIRI VIWANJANI. Thursday, November 21, - TopicsExpress



          

KWA MUKTASA YALIYOJIRI VIWANJANI. Thursday, November 21, 2013 POULSEN ATAJA 23 WATAKAOIWAKILISHA BARA KATIKA CHALENJI. KOCHA MKUU WA KILIMANJARO STARS, KIM POULSEN AMETAJA KIKOSI CHA WACHEZAJI 23 WATAKAOSHIRIKI MICHUANO YA KOMBE LA CHALENJI INAYOFANYIKA NCHINI KENYA KUANZIA NOVEMBA 27 MWAKA HUU. KILIMANJARO STARS ILIYOTWAA KOMBE HILO MARA YA MWISHO MWAKA 2010 CHINI YA KOCHA JAN POULSEN, NA AMBAYO IMEPANGWA KUNDI B KATIKA MICHUANO YA MWAKA HUU ITACHEZA MECHI YAKE YA KWANZA NOVEMBA 28 MWAKA DHIDI YA ZAMBIA KWENYE UWANJA WA MACHAKOS. WACHEZAJI WANAOUNDA KIKOSI HICHO CHA TANZANIA BARA NI MAKIPA DEOGRATIUS MUNISHI (YANGA), IVO MAPUNDA (GOR MAHIA, KENYA) NA AISHI MANULA (AZAM). MABEKI NI ERASTO NYONI (AZAM), HIMID MAO (AZAM), ISMAIL GAMBO (AZAM), KELVIN YONDANI (YANGA), MICHAEL PIUS (RUVU SHOOTING) NA SAID MORADI (AZAM). VIUNGO NI AMRI KIEMBA (SIMBA), ATHUMAN IDD (YANGA), FRANK DOMAYO (YANGA), HARUNA CHANONGO (SIMBA), HASSAN DILUNGA (RUVU SHOOTING), RAMADHAN SINGANO (SIMBA) NA SALUM ABUBAKAR (AZAM). SAFU YA USHAMBULIAJI INAUNDWA NA ELIAS MAGULI (RUVU SHOOTING), FARIDI MUSA (AZAM), JOSEPH KIMWAGA (AZAM), JUMA LIUZIO (MTIBWA SUGAR), MBWANA SAMATA (TP MAZEMBE, DRC), MRISHO NGASA (YANGA) NA THOMAS ULIMWENGU (TP MAZEMBE, DRC). KILIMANJARO STARS INATARAJIA KUONDOKA JUMATATU (NOVEMBA 25 MWAKA HUU) KWENDA NAIROBI KUSHIRIKI MICHUANO HIYO ITAKAYOANZA NOVEMBA 27 MWAKA HUU NA KUMALIZIKA DESEMBA 13 MWAKA HUU. MECHI DHIDI YA STARS, ZIMBABWE YAINGIZA MIL 50/- MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA YA FIFA DATE KATI YA TANZANIA (TAIFA STARS) NA ZIMBABWE (THE WARRIORS) ILIYOCHEZWA JUZI (NOVEMBA 19 MWAKA HUU) UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM IMEINGIZA SH. 50,980,000 KUTOKANA NA WATAZAMAJI 7,952. TIKETI ZA KUSHUHUDIA MECHI HIYO ZILIUZWA KWA SH. 5,000, SH. 10,000, SH. 15,000, SH. 20,000 NA SH. 30,000. MGAWANYO WA MAPATO HAYO ULIKUWA KAMA IFUATAVYO; ASILIMIA 18 YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) NI SH. 7,776,610.17 WAKATI WA GHARAMA ZA UCHAPAJI TIKETI NI SH. 3,682,560. ASILIMIA 15 YA UWANJA SH. 5,928,124, ASILIMIA 20 YA GHARAMA ZA MECHI SH. 7,904,166 NA ASILIMIA 5 YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA (CAF) SH. 1,976,041. ASILIMIA 60 YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) SH. 17,784,373 NA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA DAR ES SALAAM (DRFA) SH. 889,219 AMBAYO NI ASILIMIA 5 KUTOKA KWENYE MGAWO WA TFF. CHALENJI CUP-KENYA 2013: RATIBA YATOKA! Thursday, 21 November 2013 09:11 KILI STARS KUANZA NA ZAMBIA, ZANZIBAR KUIVAA SOUTH SUDAN! CECAFA CHALENJI CUP, Kombe la kusaka Nchi Bingwa ya Afrika ya Mashariki na Kati, linaanza huko Nchini Kenya Jumatano Novemba 27 kwa Nchi 12 kushindana. Nchi hizo zimegawanywa Makundi matatu ya Nchi 4 kila moja ambapo Washindi wawili wa kila Kundi watatinga Robo Fainali pamoja na Washindi wa Tatu wawili Bora. Katika Nchi hizo 12 zinazoshiriki, 11 ni Wanachama wa CECAFA, Shirikisho la Soka kwa Nchi za Afrika ya Mashariki na Kati, na moja, Zambia, ni Wageni waalikwa wa michuano hii ya Mwaka huu. Bingwa Mtetezi wa Chalenji Cup ni Uganda ambao walitwaa Kombe Mwaka Jana lilipochezwa Nchini kwao kwa kuifunga Kenya Bao 2-1 katika Fainali. Tanzania itawakilishwa na Timu mbili, yaani Kilimanjaro Stars, ambayo ni Tanzania Bara, na Zanzibar Heroes, Timu ya Zanzibar. Kili Stars wapo Kundi B na wataanza hapo Alhamisi Novemba 28 kwa kucheza na Zambia wakati Zanzibar wao wanaanza Jumanne Novemba 27 kwa kucheza na South Sudan. MAKUNDI: Kundi A KUNDI B KUNDI C -Kenya -Ethiopia -Zanzibar -South Sudan -Tanzania Bara -Zambia -Burundi -Somalia -Uganda -Rwanda -Sudan -Eritrea **FAHAMU: Timu mbili za Juu kila Kundi zitasonga Robo Fainali pamoja na Washindi wa Tatu wawili Bora. RATIBA: TAREHE NA MECHI KUNDI UWANJA SAA Jumatano Novemba 27 1 Zanzibar v South Sudan A Nyayo 1400 2 Kenya v Ethiopia A Nyayo 1630 Alhamisi Novemba 28 3 Burundi v Somalia B Machakos 1400 4 Tanzania Bara v Zambia B Machakos 1600 Ijumaa Novemba 29 5 Sudan v Eritrea C Machakos 1400 6 Uganda v Rwanda C Machakos 1600 Jumamosi Novemba 30 7 Ethiopia v Zanzibar A Nyayo 1400 8 South Sudan v Kenya A Nyayo 1600 Jumapili Desemba 1 9 Somalia v Tanzania B Nyayo 1400 10 Zambia v Burundi B Nyayo 1600 Jumatatu Desemba 2 11 Sudan v Rwanda C Machakos 1400 12 Eritrea v Uganda C Machakos 1600 Jumanne Desemba 3 13 South Sudan v Ethiopia A Machakos 1400 14 Kenya v Zanzibar A Machakos 1600 Jumatano Desemba 4 15 Tanzania v Burundi B Nyayo 1400 16 Somalia v Zambia B Nyayo 1600 Alhamisi Desemba 5 17 Rwanda v Eritrea C Nyayo 1400 18 Uganda v Sudan C Nyayo 1600 Ijumaa Desemba 6 MAPUMZIKO ROBO FAINALI Jumamosi Desemba 7 19 C1 v B2 Mombasa BADO 20 A1 v 3 BORA 1 Mombasa BADO Jumapili Desemba 8 21 B1 v 3 BORA 2 Mombasa BADO 22 A2 v C2 Mombasa BADO Jumatatu Desemba 9 MAPUMZIKO Jumanne Desemba 10 NUSU FAINALI 23 Mshindi 19 v Mshindi 20 BADO 24 Mshindi 21 v Mshindi 22 BADO Jumatano Desemba 11 MAPUMZIKO Alhamisi Desemba 12 25 Mshindi wa Tatu 1400 26 FAINALI 1600 KATIKA ANGA ZA KIMATAIFA BARCELONA KUWAKOSA MESSI NA VALDES MWAKA HUU. MABINGWA WATETEZI WA LIGI KUU NCHINI HISPANIA, BARCELONA ITALAZIMIKA KUCHEZA MECHI ZAO NANE ZILIZOSALIA KWA MWAKA HUU KUANZIA MECHI YA JUMAMOSI DHIDI YA GRANADA BILA YA MSHAMBULIAJI WAKE MAHIRI LIONEL MESSI NA GOLIKIPA VICTOR VALDES. MESSI YUKO KITANDANI AKIUGUZA MSULI WA NYUMA YA PAJA LA MGUU WAKE WA KUSHOTO WAKATI VALDES AMBAYE AMEKUWA KATIKA KIWANGO CHA JUU MSIMU HUU NAYE AMECHANIKA MSULI WA MGUU WAKE WA KULIA. KAMA HIYO HAITOSHI, KUINGO MCHEZESHAJI WA TIMU HIYO XAVI HERNANDEZ NAYE KUNA HATI HATI YA KUUKOSA MCHEZO WA JUMAMOSI KUTOKANA NA MAJERAHA YA MSULI WA KIGIMBI NA JORDI ALBA NAYE BADO YUKO KITANDANI AKIJIUGUZA. HATA HIVYO MAJERUHI HAYAWEZI KUIBABAISHA KLABU HIYO KUTOKANA NA HISTORIA YA NYUMA KWANI VALDES NA MESSI WAMEWAHI KUKOSEKANA KATIKA KIKOSI KWA MUDA UNAOFANANA MWAKA 2007 NA TIMU HIYO KUFANIKIWA KUSHINDA MECHI 13 KATI YA 16 WALIZOCHEZA BILA YAO. GUARDIOLA APATA AHUENI BAADA YA BOATENG KUWA FITI TAYARI KWA DORTMUND. KOCHA WA KLABU YA BAYERN MUNICH PEP GUARDIOLA AMEPATA HABARI NJEMA KUTOKA KATIKA MEZA YA MADAKTARI WA TIMU HIYO KUELEKEA KATIKA MCHEZO WA MWISHONI MWA WIKI DHIDI YA MAHASIMU WAO BORUSSIA DORTMUND. MADAKTARI WA TIMU HIYO WAMEMHAKIKISHIA KOCHA HUYO KWAMBA BEKI WAKE TEGEMEO JEROME BOATENG ANATAKUWA FITI KWA AJILI YA MCHEZO HUO MUHIMU WA BUNDESLIGA. BEKI HUYO WA KATI ALIUMIA KISIGINO WAKATI AKIITUMIKIA UJERUMANI KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI WA KIMATAIFA DHIDI YA UINGEREZA AMBAO WALISHINDA KWA BAO 1-0 NA BAYERN WALIKUWA NA HOFU NYOTA HUYO KUKOSEKANA KATIKA MCHEZO HUO WA JUMAMOSI. HATA HIVYO, BOATENG MWENYE UMRI WA MIAKA 25 ALITHIBITISHA KUWA ATAKUWEPO KATIKA MCHEZO HUO UTAKAOPIGWA KATIKA UWANJA WA SIGNAL IDUNA PARK JIJINI DORTMUND. KATIKA MCHEZO HUO BAYERN WATAKUWA WAKISAKA USHINDI ILI KUONGEZA PENGO LA ALAMA KUFIKIA NNE KATIKA MSIMAMO WA BUNDESLIGA WAKATI WAPINZANI WAO WATAKUWA WAKIPAMBANA ILI KUHAKIKISHA WANABAKISHA PENGO LA ALAMA MOJA BAINA YAO. ALVES AMFAGILIA RONALDO KUCHUKUA BALLON DOR. BEKI MAHIRI WA KLABU YA BARCELONA, DANI ALVES AMEKIRI KUWA MSHAMBULIAJI WA REAL MADRID CRISTIANO RONALDO YUKO KATIKA KIWANGO BORA KULIKO HASIMU WAKE KATIKA TUZO ZA BALLON D’OR LIONEL MESSI NA FRANCK RIBERY LAKINI ANAFIKIRI KUKOSA TAJI LOLOTE KWA RONALDO MSIMU HUU KUNAWEZA KUMGHARIMU KUIKOSA TUZO HIYO. RONALDO MWENYE UMRI WA MIAKA 28 AMEKUWA KATIKA KIWANGO CHA JUU TOKA KUANZA KWA MSIMU WA 2013-2014, AKIWA AMEFUNGA MABAO 24 KATIKA MECHI 17 ALIZOCHEZA HUKU AKIFUNGA MABAO MENGINE MANNE YALIYOIWEZESHA URENO KUKATA TIKETI YA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2014. WAKATI AKIKIRI KIWANGO KIKUBWA CHA NYOTA HUYO, ALVES ANAAMINI KUWA KUKOSA TAJI LOLOTE KWA MADRID KATIKA MSIMU WA 2012-2013 KUTAMUWEKA KATIKA NAFASI MBAYA KWENYE TUZO HIZO. ALVES AMESEMA KARATA YAKE INAKWENDA KWA MESSI AU RIBERY NA KAMA SIO MESSI BASI ANAYESTAHILI TUZO HIYO NI RIBERY KWASABABU AMESHINDA KILA NA ALIKUWA MHIMILI MUHIMU KWA TIMU YA BAYERN MUNICH. ORODHA KAMILI YA TIMU 32 ZILIZOFUZU KOMBE LA DUNIA 2014. URUGUAY IMEKUWA TAIFA LA MWISHO KUKATA TIKETI YA KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2014 ZITAKAZOPIGWA NCHINI BRAZIL BAADA YA KUTOKA SARE YA 0-0 NA JORDAN KATIKA MCHEZO WA MKONDO WA PILI HATUA YA MTOANO. URUGUAY KATIKA MCHEZO WA KWANZA WALIPATA USHINDI WA MABAO 5-0 NA KATIKA MCHEZO HUO WA PILI ULIOPIGWA JIJINI MONTEVIDEO WALITAWALA SEHEMU KUBWA YA MCHEZO NA WALIKARIBIA KUFUNGA BAADA YA KICHWA KILICHOPIGWA NA DIEGO GODIN KUGONGA MLINGOTI. NCHI HIYO YA AMERICA KUSINI AMBAO KWASASA WANAKAMATA NAFASI YA SITA KWENYE UBORA WA VIWANGO VYA DUNIA WALISHINDA TAJI HILO 1930 NA 1950 NA WAKAFIKA NUSU FAINALI KWENYE FAINALI ZILIZOPIGWA NCHINI AFRICA KUSINI 2010. ORODHA KAMILI YA TIMU 32 ZITAKAZOSHIRIKI MICHUANO HIYO KWA UPANDE WA BARA LA AFRIKA NI ALGERIA, CAMEROON, GHANA, IVORY COAST, NIGERIA, BARA LA ASIA NI AUSTRALIA, IRAN, JAPAN NA KOREA KUSINI WAKATI ULAYA ITAWAKILISHWA NA UBELGIJI, BOSNIA-HERCEGOVINA, CROATIA, UINGEREZA, UFARANSA, UJERUMANI, UGIRIKI, ITALIA, UHOLANZI, URENO, URUSI, SWITZERLAND NA HISPANIA. NYINGINE NI COSTA RICA, HONDURAS, MEXICO NA MAREKANI AMBAZO ZINAWAKILISHA NCHI ZA AMERIKA KASKAZINI, KATI NA CARIBBEAN HUKU BARA LA AMERIKA KUSINI LIKIWAKILISHWA NA ARGENTINA, BRAZIL AMBAO NI WENYEJI, COLOMBIA, ECUADOR, CHILE NA URUGUAY. FIFA KUTUMIA SPRAY MAALUMU KATIKA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA. SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI-FIFA LIMEPANGA KUTUMIA KUTUMIA SPRAY MAALUMU KATIKA SEHEMU YA MSTARI WA UKUTA KABLA YA KUPIGWA ADHABU KWENYE MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA ILI KUWARAHISISHIA WAAMUZI. KATIKA TAARIFA YAKE FIFA IMESEMA SPRAY HIYO ITATUMIKA KWENYE MICHUANO HIYO ITAKAYOANZA KUTIMUA VUMBI DECEMBER 11-21 NCHINI MOROCCO BAADA YA KUFANYIWA MAJARIBIO KWENYE MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KWA VIJANA CHINI YA MIAKA 17 NA 20. SPRAY HIYO AMBAYO HUPOTEA BAADA YA DAKIKA MOJA ITAKUWA INAPULIZWA UWANJANI KUCHORA MSTARI WA KUPANGA UKUTA WA TIMU INAYOPIGIWA ADHABU, KITU AMBACHO KITAONDOA KADI ZA NJANO AMBAZO HUPEWA MCHEZAJI ANAYEKAIDI MAAMUZI YA MWAMUZI YA KUONESHA SEHEMU YA KUWEKA UKUTA WA KULINDA LANGO LAO. KLABU BINGWA YA DUNIA YA VILABU ITAZIHUSISHA BAYERN MUNICH YA UJERUMANI, ATLETICO MINEIRO YA BRAZIL, GUANGZHOU EVERGRANDE YA CHINA, AL AHLY YA MISRI, MONTERREY YA MEXICO, AUCKLAND CITY YA NEW ZEALAND NA RAJA CASABLANCA YA MOROC TIMU AMBAZO ZIPO FAINALI KOMBE LA DUNIA BRAZIL [JUMLA 32]: AFIKA [NCHI 5]: NIGERIA, IVORY COAST, CAMEROUN, GHANA, ALGERIA EUROPE [NCHI 13]: BELGIUM, BOSNIA-HERZEGOVINA, ENGLAND, GERMANY, ITALY, NETHERLANDS, RUSSIA, SPAIN, SWITZERLAND, PORTUGAL, FRANCE, CROATIA, GREECE SOUTH AMERICA [NCHI 6]: ARGENTINA, BRAZIL (WENYEJI), CHILE, COLOMBIA, ECUADOR, URUGUAY ASIA [NCHI 4, JORDAN WAPO KWENYE MCHUJO]: AUSTRALIA, IRAN, JAPAN, SOUTH KOREA NORTH & CENTRAL AMERICA/CARIBBEAN [NCHI 4]: COSTA RICA, HONDURAS, USA, MEXICO ++++++++++++++++++++++++++ INGAWA DROO MAALUM YA KUPANGA MAKUNDI ITAFANYIKA DESEMBA 6 HUKO COSTA DO SAUÍPE RESORT, MATA DE SÃO JOÃO, BAHIA, BRAZIL, TAYARI WADADISI WA MAMBO WAMESHAKUJA NA UPANGAJI WAO WA TIMU KWENYE VYUNGU KWA AJILI YA DROO HIYO AMBAPO ITAKUWA NA VYUNGU VINNE. CHUNGU CHA KWANZA NI KILE CHA TIMU BORA DUNIANI KWA MUJIBU WA LISTI YA FIFA YA UBORA DUNIANI NA HIZO NI SPAIN, BRAZIL [WENYEJI AMBAO WASHAPANGWA KUNDI A], GERMANY, ARGENTINA, COLOMBIA, BELGIUM, SWITZERLAND NA URUGUAY. VYUNGU VINGINE VITATU PIA VITAKUWA NA TIMU 8 KILA MOJA NA HUMO HULUNDIKWA TIMU TOKA BARA MOJA AU KANDA MOJA ZILIZO NA UBORA WA JUU. KWENYE DROO, KITAKACHOFANYIKA NI KUTOA TIMU MOJA TOKA KILA CHUNGU NA KUUNDA KUNDI MOJA AMBAPO KUTAKUWA NA MAKUNDI MANNE YA TIMU 4 KILA MOJA. KWA MUJIBU WA WADADISI HAO, VYUNGU VITAKUWA KAMA IFUATAVYO: [ONYO: HII SI RASMI KWA MUJIBU WA FIFA-NI UWEZEKANO TU!!] -CHUNGU NAMBA 1: SPAIN, BRAZIL [WENYEJI AMBAO WASHAPANGWA KUNDI A], GERMANY, ARGENTINA, COLOMBIA, BELGIUM, SWITZERLAND NA URUGUAY -CHUNGU NAMBA 2: HOLLAND, ITALY, ENGLAND, PORTUGAL, GREECE, BOSNIA, CROATIA, RUSSIA -CHUNGU NAMBA 3: FRANCE, CHILE, ECUADOR, NIGERIA, CAMEROON, IVORY COAST, ALGERIA, GHANA -CHUNGU NAMBA 4: JAPAN, AUSTRALIA, IRAN, SOUTH KOREA, COSTA RICA, USA, MEXICO, HONDURAS ++++++++++++++++++++++++++ **FAHAMU: -RATIBA IMESHATOKA BOFYA HAPA: - DROO YA KUPANGA MAKUNDI: -KUFANYIKA TAREHE 6 DESEMBA 2013 COSTA DO SAUÍPE RESORT, MATA DE SÃO JOÃO, BAHIA, BRAZIL -KWENYE DROO HIYO TIMU 7, PAMOJA NA BRAZIL, AMBAZO ZIKO JUU KWENYE LISTI YA FIFA YA UBORA DUNIANI ZITAWEKWA CHUNGU NA 1 NA TIMU NYINGINE 24 ZILIZOBAKIA ZITAGAWANYWA NANE NANE NA KUINGIZWA VYUNGU VINGINE VITATU NA KUTENGANISHWA KUTOKA MABARA ZINAKOTOKA. -FAINALI KUCHEZWA: 12 JUNI 2014 HADI 13 JULAI 2014 ++++++++++++++++++++++++++
Posted on: Thu, 21 Nov 2013 13:24:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015