SIKUYAFURAHIA SANA MATEMBEZ YA KUPINGA KUUAWA KWA TEMBO YA PALE - TopicsExpress



          

SIKUYAFURAHIA SANA MATEMBEZ YA KUPINGA KUUAWA KWA TEMBO YA PALE ARUSHA Ni Tanzania yetu na maajabu yanayoendelea.Kama si babu wa Samunge ni mabomu,kama si kuuawa kwa Albino ni mwehu Mtesa Ulimboka kule Magwepande na sasa ni kituko cha tukusanya watz eti matembez ya kupinga kuuawa kwa Tembo.Ni nani asiyefahamu kuwa meno ya Tembo ndiyo yamewatajirisha vigogo wengi ambao daima kwa kuwinda haram kumewajengea nguvu kuliko hata mkono wa dola? Nani anasahau kuwa tembo wamesababisha vilio kwa wananchi ambao licha ya mazao yao kuharibiwa na Tembo wamepoteza hata ndug zao kwa kujeruhiwa na Tembo.si Maana yangu hata kidogo kwamba wanyama hawa wauawe lakini hofu yangu ni kama matembez yale ya Arusha ni ridhaa ya wananchi na kama ni kweli watz leo wameona na kufaidika na wanyama hawa.Niombe kutofungwa mdomo kuwa matembez yale ya Arusha yanayopinga kuuawa kwa tembo yanalenga kuwalinda wale wakwasi Mabwana Wakubwa Kutopolomosha Utajiri Wao.Tumeshindwaje kufanya matembez kulilia waliouawa kwa Mabom Aru?
Posted on: Sat, 05 Oct 2013 17:24:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015