WATANZANIA 35 WASEKWA GEREZAN NCHINI PAKISTAN KWA TUHUMA ZA MADAWA - TopicsExpress



          

WATANZANIA 35 WASEKWA GEREZAN NCHINI PAKISTAN KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA Taarifa iliyotolewa juzi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, ilisema Watanzania hao wanashikiliwa kutokana na kujihusisha na makosa mbalimbali. Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Buruhani, amesema kuwa Watanzania hao wanashikiliwa kutokana na makosa mbalimbali, yakiwamo ya kukutwa na dawa za kulevya, wizi wa mali za umma, kuishi Pakistan bila kibali na kutokuwa na hati za kusafiria. “Katika taarifa yetu ya awali hatukutoa sababu, lakini kutokana na kuhojiwa na waandishi wengi tumelazimika kutoa sababu ambapo tuliwataka wazazi, ndugu na jamaa wajitokeze hapa kwetu ili watoe ushirikiano kwa lengo la kufanikisha kuwarejesha nchini.“Raia hawa walianza kwenda nchini Pakistan kuanzia miaka ya 1989 na hujulikana ni raia wa Tanzania, baada ya kufanya makosa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. “Kwa hawa raia walio katika magereza hayo, walihukumiwa kuanzia miaka ya 2003 hadi mwaka jana, wengine wamemaliza vifungo vyao hivyo hawawezi kuachiwa mpaka wakabidhiwe kwenye nchi husika. “Hawa wanaotakiwa kurudishwa nchini, ni wale waliomaliza kutumikia vifungo vyao, kuna wengi walihukumiwa kulipa faini, lakini kutokana na kutokuwa na ndugu, walitumikia kifungo. “Tumechunguza umri wao na miaka waliyokaa huko, tumegundua walikwenda wakiwa na umri wa vijana kati ya 25 hadi 30 na biashara yao ilikuwa ni dawa za kulevya, pengine tayari wametengeneza familia isiyo halali nchini humo,” alisema. Alisema idara yake imeshindwa kuweka mawasiliano ya moja kwa moja na ndugu wa raia wanaoshikiliwa, kwa sababu ya kukwepa usumbufu. Watanzania wanaoshikiliwa Pakistan ni Usma Mdoe, mzaliwa wa Tanga, Hemed Himji (Dar es Salaam), Mbwana Eka (Zanzibar), Furahisha Seif (Dar es Salaam), Omar Twaha (Mwanza), Alamgiri Akbar (Dar es Salaam), Abubakar Khamis (Tanga), Mohamed Abdul (Tanga), Mohamed Mohamed (Tanga) na Ali Kipuya (Dar). Wengine ni Ashraf Zakhy (Tanga), Mwinyi Mwinyigoha (Pwani), Athuman Singano (Tanga), Abubakar Ally (Zanzibar), Said Mohamed (Dar es Salaam), Omar Suleiman (Pwani), Abdullah Rayngul (Lindi), Jamal Jaffar (Dar es Salaam), Frank Kimweri (Dar es Salaam), Rajab Simbaulaya (Dar es Salaam), Hafdh Sharif (Tanga), Juma Chonanga (Dar). Pia wamo, Mohamed Juma (Zanzibar), Hassan Mohamed (Dar es Salaam), Bonane Dilunga (Dar es Salaam), Rajab Msalagala (Tanga), Mansoor Kaswamba (Dar es Salaam), Ally Said (Tanga), Mohamed Bashiri (Dar es Salaam), Uruka Malipula (Morogoro), Seif Seif (Zanzibar), Shaaban Mussa (Dar es Salaam), Said Madelelia na Rashid Sambatora (Dar es Salaam). Alisema Watanzania wamekuwa na tabia kukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta maisha, bila kufuata taratibu zinazotakiwa. Alisema wengi wao, wamekuwa na tabia ya kukimbilia nchi za Afrika Kusini, Pakistan, Botswana na nchi nyingine ambazo ni jirani.
Posted on: Thu, 27 Jun 2013 13:21:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015