katika sports oanel siku ya leo utaenda kusikia mengi zaidi lakini - TopicsExpress



          

katika sports oanel siku ya leo utaenda kusikia mengi zaidi lakini ni pamoja na Watanzania watatu ni miongoni mwa washiriki 30 walioteuliwa kuhudhuria kozi ya wakufunzi ya waamuzi ya FUTURO III itakayofanyika Addis Ababa, Ethiopia kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya miaka 20 Kanda ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji. KIUNGO chipukizi Mtanzania, Adam Nditi amepandishwa kutoka timu ya akademi ya Chelsea ya England hadi timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21- maana yake akifanya vizuri wakati wowote anaweza kupandishwa rasmi kikosi cha kwanza. Na, YALE Mashindano ya ngazi ya chini ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI, leo Usiku yapo kilingeni kwa Mechi za Pili za Makundi. Yapo Makundi 12 ya Timu 4 kila moja na Wawakilishi wa England ni Tottenham, waliomaliza Nafasi ya 4 Ligi Kuu England Msimu uliopita, Swansea City, Mabingwa wa Capital One Cup na Wigan Atletics, Mabingwa wa FA CUP. ungana nami kocha mchezaji RICHIE FLAVOUR KARIBU NYOTE
Posted on: Thu, 03 Oct 2013 16:28:55 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015