mimi ni shabiki wa simba damu,ata mama yangu anajua,lakini kitendo - TopicsExpress



          

mimi ni shabiki wa simba damu,ata mama yangu anajua,lakini kitendo walichofanya mashabiki njaa wa simba,waliolaaniwa na wazazi wao pamoja na Mungu sikubaliani nacho hata kidogo na nakilaani,hakuna asiyejua kama timu yetu ni mbovu kwasasa na ile droo tuliyotoa na Yanga tusijivunie na kuvimbisha vichwa eti tuna team la,tukumbuke mechi ya watani huwa ina mambo mengi sana zaidi ya mpira wenyewe,kwahiyo haiwezi kupima kiwango chetu halisi,timu za kupima kiwango chetu ndio kama hizi Azam,Coastal na Kagera sugar,mechi zote hizo hatujashinda hata moja,timu kama kagera tungeipiga goli 3 hiyo penalti ingewasaidia nini? wamepata moyo wa kushambulia kwasababu tulikuwa na kagoli kamoja...Jamani wana SIMBA wenzangu imefika wakati tukubali kama hatuna timu kwasasa,kama YANGA wananunua mechi vipi kuhusu MBEYA CITY?? SIMBA timu yetu ni mbovu tukubali tu....
Posted on: Fri, 01 Nov 2013 13:37:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015