story: NALILIA PENZI sehemu: 1 Ilikuwa Ijumaa tulivu - TopicsExpress



          

story: NALILIA PENZI sehemu: 1 Ilikuwa Ijumaa tulivu iliyotawaliwa na jua kali ndani ya jiji la Mwanza maeneo ya chuo cha CBE karibu kabisa na jengo maarufu jijini hapo la PPF Plaza. Ilikuwa majira ya saa 9 alasili muda ambao mwanadada mrembo wa Kinyamwezi, alikuwa akielekea pembeni kidogo ya chuo hicho katika maktaba kuu ya mkoa huu. Msichana mwenye mwonekano wa kipekee chuoni hapo na huenda ikawa pia ndani ya jiji hili zima la miamba. Aliyejaliwa macho mazuri yasiyokuwa na hitaji la kuweka chochote ili yalembue kwa watoto wa mjini wanayaita "macho ya kusinzia" mwenye sura inayovutia hasa pale anapoachia tabasamu ambalo huwachanganya wanaume wengi wanaobahatika kuliona kutokana na mashimo yanayotokea katika mashavu yake kwa wajanja yanajulikana kama "Dimpozi" na nafasi inayopatikana katikati ya meno yake katika kinywa chake ambayo nayo hujulikana kama "Mwanya". Shingo inayovutia iliyobeba kichwa chenye ukubwa wa kulingana na mmiliki mwenyewe huku shingo hiyo ikiwa imebebwa na mwili ulioumbwa ukaumbika kuanzia unyayo wa miguu mpaka sehemu ya mabega yaloungana na shingo hiyo. Katikati ya mwili wake ama kiunoni alikuwa na ujazo unaoridhisha kabisa chini ya mgongo wake na miguu iliyositahili kabisa kuubeba mwili huo. Huyu ni msichana mdogo tu mwenye umri wa miaka 24 aliyetoka katika familia ya mzee KILONA maarufu kama Mzee Kilo na mkewe Rebeka walobahatika kupata watoto wawili tu wote wa kike. PAULINE kama dada mkubwa mwenye umri wa miaka 28 aliyeajiriwa na benki ya NBC tawi dogo katika manispaa ya Tabora na PENDO kama mdogo akiwa ni mwanafunzi katika chuo cha CBE tawi la mkoa wa Mwanza. "Pennn..." alisikia sauti ikimuita wakati akivuka barabara kueleke upande wa pili ilipo maktaba hiyo ya mkoa. Alipogeuka aligundua ilikuwa ni sauti ya Tony mpenzi wake, "vipi bado unaenda kukaza" aliuliza Tony, "No, napeleka hiki kitabu mara moja afu ndo niende hom, vipi leo tunaongozana?" Alijibu na kuongeza swali Pendo ama Pen kama ilivyozoeleka kwa watu wake wa karibu. "No,naingia posta mara moja then ntakuja uko" "Nikuandalie nini leo" aliuliza Pen huku akitoa tabasam lililomfanya Tony achelewe kujibu na kubaki amekodoa macho kumwangalia Pen. "chochote tu ulichopanga kula leo" alijikuta anajibu baada ya Pen nae kumkazia macho. "poa,leo mi nimepanga kula ugali na samaki" "Itakuwa poa,manake na mda mrefu sijala samaki. Twende nikusindike si unarudisha tu kitabu" "Yah!" alijibu Pen uku wakiongozana.. "sasa mi ngoja nipitie ivi mwanza hotel nikamcheki mshikaji afu ndo niende posta" "poa,mi ngoja nikapande daladala,ila usiache kuja maana naenda kusonga bonge la ugali" aliongea Pen kama masihara uku wakiagana na kila mmoja kuchukua uelekeo wake.. Baada ya kutembea hatua kadhaa mara Pen alisikia kelele za watu wakiashiria ajari imetokea. Alipogeuka na kukimbia kuangalia ni nini kimetokea, alipigwa na butwaa alipoiona shati alokuwa kavaa Tony ipo chini barabarani uku mbele yake kukiwa na gari maarufu kama Tax imesimama. "Mungu wangu Tony" Pen alijikuta anapiga yowe huku akielekea mahari pale. Ni tukio la chini ya dakika 5 lakini watu walikuwa wamejaa balaa. Alipofika na kumgeuza kichwa Tony alikuwa anatokwa damu puani na mdomoni uku suruali kwa upande wa mguu wa kushoto nayo ukiwaimelowa damu... * * * Utamu ndo umeanzia hapo, nini kitajiri. Je, Tony ndo kamuacha Pen ki ivyo ama vipi.. Tukutane kesho .usiku mwema.
Posted on: Fri, 02 Aug 2013 21:02:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015