Alikuja bwana mmoja kwa Imam Shafii Rahimahullah akamwambia kuwa - TopicsExpress



          

Alikuja bwana mmoja kwa Imam Shafii Rahimahullah akamwambia kuwa maisha ni magumu na anachopata hakimtoshi kuangalia familia yake anapata dirham tano kama mshahara wake na hautoshi, Imam Shafii akamwambia nenda ukamwambie tajiri yako akupunguzie mshahara wako uwe dirham nne, yule bwana akashangaa lakini ikambidi aende na akapunguziwa.. Baada ya mda akarudi tena akilalamika hali ile ile, Imam Shafi akamwambia nenda ukamwambie tajiri yako akupunguzie akupe dirham tatu, akashangaa ikabidi aende tuu na akapunguziwa.. Baada ya mda akaja kwa Imam Shafii na furaha sana akimwambia kuwa dirham tatu zamtosha yeye na familia yake.. Imam Shafii akamwambia kuwa kazi unayofanya inastahiki dirham tatu tuu, zile dirham mbili za juu sio haki yako ndio sababu ya kukimbiza barka katika kipato chako.. Kisha akasema kukusanya haraam na halaal pamoja, inaipa nafasi haraam kuingia kwa halaal na kukosesha baraka
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 09:06:33 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015