CHADEMA UK inaendelea hapa. 3. Tumetuma barua kwenye balozi zaidi - TopicsExpress



          

CHADEMA UK inaendelea hapa. 3. Tumetuma barua kwenye balozi zaidi ya nane za nchi mbali mbali tukiyaeleza na kuyaanisha matukio yanayoendelea ndani ya nchi huku viongozi wetu wakikaa kimya. 4. Tumevitaarifu vyombo mbali mbali vya habari kama vile BBC, RT Television na Aljazeer kuhusu hali na mwelekeo wa kisiasa Tanzania ambao umeanza kuchukua sura mpya. Kwa nguvu zote tutaendelea kuueleza ulimwengu na kukaripia uhalifu huu tunaofanyiwa ndani ya nchi. Ni muhimu kwa waTanzania kufahamu kwamba upinzani siyo dhambi . Upinzani ni mawazo mbadala. Kwa wana-CHADEMA wenzetu Tanzania ni nchi yetu tunayoipenda na kuithamini. Tunaamini kabisa kwamba amani na utulivu ni vitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Sote tunatamani kuwarithisha watoto wetu (next generation) nchi itakayowapa fursa ya kusonga mbele. Hata hivyo amani tunayoiongelea hapa si amani ambayo tumeaminishwa na serikali ya ccm kwa miaka mingi. Amani tunayoisema ni amani ya kweli, amani inayoheshimu utu, amani inayompa fursa kila mwananchi kufanya shuughuli zake bila kuogopa ili mradi anafuata sheria za nchi. Ni dhahiri kwamba wengi tumechoshwa na uongozi mbovu ambao tumeifikisha nchi hii hapa tulipo leo. Wengine hata tunashangaa kwamba hawa hawa ambao wamekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 50 bila kuleta maendeleo yeyote, leo hii wanaonekana kutaka kung’ang’ania madaraka kwa gharama zozote zile hata kwa kumwaga damu. Watu hawa wanaonesha uchu na jazba ya hali ya juu lakini wakiambiwa wajieleze ni nini wamekifanya kwa miaka 50 hawana jibu. Ikiwa kama haitoshi, wengi tunaona kwamba sasa imetosha, tumeshavumilia vya kutosha (enough is enough). Pamoja na hayo tunawaomba wanaCHADEMA wote kuendelee kutetea bila kuchoka juhudi za kulikomboa taifa letu. Juhudi hizi zitazaa matunda siku siyo nyingi. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Nchi Yetu --------------------------------- Habari na Uenezi - CHADEMA UK [email protected] CHADEMA UK
Posted on: Fri, 21 Jun 2013 13:23:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015