HABARINI WADAU KAMA KAWAIDA LEO NDO SIKU ILE AMBAYO TUNAANZA NA - TopicsExpress



          

HABARINI WADAU KAMA KAWAIDA LEO NDO SIKU ILE AMBAYO TUNAANZA NA STORY YETU TOLEO LA #PILI. JINA LA STORY--#UKUBWA_DAWA. MTUNZI---#mfikwa j #TULIPO ISHIA SEHEMU YA KWANZA Polisi walipomaliza kukamata eneo lile watuhumiwa wote walipelekwa kwanza kituo cha polisi kwa maojiano zaidi ili wapelekwe mahakamani. #ENDELEA K2 kuona rafiki yake amekamatwa na Polisi na yeye amefanikiwa kukimbia akawa hana la kufanya kwa muda ule maana alikuwa ajui pwa kwenda pia pale kigoma ni mgeni.Akiwa amechoka sana huku akiwa amekaa nyuma nyumba ya watu ndipo akapita mama moja na kumkuta K2 yupo pale ameduaa yule mama alimsalimia K2 kijana habari yako lakini K2 akujibu chochote huku akiwa anamwangalia yule mama zilipita kama dakika tano au sita yule mama akagundua kuwa huyu kijana ana msongo wa mawazo ndipo alipo mshika na kumwambia kijana unaumwa kitendo kile kilimfanya K2 ajikute analopoka mimi siyo mimi siyo mimi ni mgeni tu hapa kigoma yule mama akashtuka kisha akamwambia kijana unamatatizo gani baada ya muda K2 akili kukaa sawa ndipo akaanza kumsimulia yule mama yaliyomkuta.JJ baada ya kufikishwa kituo cha polisi kwa maojiano gari ya polisi ilifika kituo kikubwa cha polisi watuhumiwa wote wakashuka na kuingizwa kituoni baada ya muda mfupi alitokea mkuu wa kituo na kuwaamulu wale askari kuwapekua na kuwaingiza lock up bila kuchelewa JJ na wenzake sita walipelekwa lock up wakisubiri ni nini kitafuata dhidi yao walikaa mahabusu mpaka kesho yake yani siku inayofuata walilala kulivyo kucha majira ya saa mbili ndipo walipoanza kuojiwa waliojiwa watuhumiwa wote ilipofika zamu ya JJ kupelekwa kwa mkuu wa upelelezi ndipo alipo jitetea kuwa yeye ni mgeni pale kigoma ametokea iringa ameenda kigoma kumtafuta kaka yake mkubwa aliyekuwa kigoma miaka kadhaa iliyopita baada ya maojiano yale mkuu wa upepelezi aliwarudisha mahabusu. Wakiwa mahabusu wa wale vijana sita ndipo kijana mmojakati ya wale sita akaanza kumlaumu mwenzie JUMA nilikwambia ukawa mbishi bora tulivyo kuwa Kongo tulikuwa tunapata pesa kiasi umenileta kigoma ili tufungwa ona sasa hatuna ata ndugu huku tutafanyaje? yule JUMA akiwa hana na kusema ndipo JJ akamuuliza yule jamaa aliyekuwa analalamika kwani nyinyi kongo mlikuwa mnafanya shughuli gani mpaka mkaja kigoma na yakawakuta haya yule jamaa akamwambia mshikaji kongo sisi tulikuwa tunachimba madini na tulivyoona kazi ya madini ni ngumu ilibidi tuje kigoma kutafuta kazi nyingine kama tungepata. Yle mama na K2 walitoka pale mpaka kwa yule mama nyumbani kwake K2 alikaribishwa mpaka ndani akapewa chakula akiwa anakula ngipo akaingia askari akiwa amevaa sare za polisi K2 aliogopa sana yule askari kuingia tu akamfata alipokaa K2 na kumwambia kijana habari yako huku K2 akiwa hana cha kujibu akatokea yule mama na kumwambia ehh mume wangu umerudi tayari pole na kazi mume wangu na pale nilivyokupigia simu kukwambia kuhusu yule kijana ndo huyu K2 akiwa hana la kusema jasho jembamba likawa linamtoka pale akajua na yeye ndo amekuja kukamatwa baada ya kusema vile yule mama akamwambia K2 huyuni mume wangu ni mkuu wa kituo hapa kigoma na dhani atakusaidia kumpata ndugu yako lakini kwa sasa hutakaa hapa sawa kijana K2 akamwambia yule mama kwa kusitasita sawa nitashukuru baada ya pale yule askari akiwa anaongea na K2 na kumuuliza maswali ya hapa na pale K2 akamwambia kila kitu yule askari na kuwa ana ndugu yake kakamatwa mchana wa leo stend ya mabasi ya mikoani yule askari akamwambia kuwa kesho asubuhi akienda kazini atafanya mpango amlete yule rafiki yake. Ilikuwa jioni kama saa kumi na moja yule mukuu wa upelelezi baada ya kubaini wale vijana walio kamwatwa stendi hawana hatia ndipo alipowatowa waende zao baadaya kutoka wale vijana kila mmoja akaanza kuondoka kivyake JJ akiwa hajui aende wapi ikabidi hawafate wale vijana walio kuwa wanazozazana mule mahabusu kama hatua kumi au ishirini wale vijana wawili walisikia sauti inawaita nyuma yao juma juma walipogeuka wakamkuta JJ anawafata wakiwa wanatembea wale vijana kwaanza kumuuliza ndugu unataka nini maana sisi tunataka kwenda kongo maana hapa kigoma tumeona ni mikosi tu na JJ kwa kuwa anatafuta maisha nae akasema kwa kuwa na mimi natafuta maisha twendeni wote huko huko tupo walipotambulishana wale vijana na kuondoka maeneo yale ili kesho yake waanze safari ya kwenda nchi ya jirani kongo.Asubuhi ilipofika mara K2 akakuta mlango unagongwa kwenye chumba alichokuwa amelala alipoamka na kufungua mlango akamkutayule askari huku akiwa amevaa nguo za kipolisi kijana habari yako K2akajibu salama shikamoo yule askari akamwambia marahaba sasa mimi naondoka naenda kazini nikifika kazini nitajua ni jinsi gani ya kumsaidia ndugu yako ili nirudi nae baadae sawa K2akamwambia yule askari sawa nimekuelewa nitashukuru sawa baada ya kumwambia vile yule askari akaondoka na kuelekea kazini. Mkuu wa kituo kuingia ofisini akamwita askari aliyoko kaunta na kumwambia kuwa amletee mahabusu mmoja anaitwa JJ yule askari akatoka mpaka chumba cha mahabusu alipoulizia jina hilo wale mahabusu walio kuwa mle ndani wakamwambia ametoka jana saa kumi jioni yule askari ikabidi aende kumwambia mkuu wa kituo kuwa tayari ametoka ameeachiwa huru yule mkuu wa kituo baada ya kupewa taarifa hizo ikabidi ampigie mke wake nyumbani na kumwambia kuwa tayari ameachiwa baada ya taarifa zile yule mama ikabidi amwambie K2 kuwa ndugu yako tayari ametoka kituoni lakini aijulikani alipoenda K2 akiwa ajui ajibu nini baada ya taarifa zile akamwambia yule mama ngoja nikamtafute basi yule mama akamwambie wewe kigoma hii ni kubwa utamtafutia wapi subiri mume wangu akirudi atajua ataklusaidiaje sawa mwanangu K2 ikabidi awe mpole.Siku iliyo kuwa inasubiliwa ilifika safari ya wale vijana akiwepo na JJ akaanza walifika ziwani tanganyika na kupanda mtumbi kuelekea kongo wakiwa katikati ya majini wale vijana wawili wakamwambia JJ kuwa tunakoenda ni hatari sana maana kuna baadhi ya sehemu tutapia kuna kambi za waasi sasa basi inabidi uwe mjanja sana maana wakikukamata wanakuua au kukufanya chochote wanachokitaka wao sawa rafiki JJ akiwa ameduwaa hana la kujibu moyo wa ujasiri ukamtuma aseme nyinyi ywendeni mungu ndo anapanga.#Itaendelea+ Je JJ na wale vijana watafanikiwa walipokusudia kwenda na je K2 atachukua maamuzi gani kama asipo muona rafiki yake. #USIKOSE TOLEO LA TATU SIKU YA KESHO
Posted on: Fri, 04 Oct 2013 05:41:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015