HIVI TANZANIA BILA USANII HAIWEZEKANI..? Kweli sikio la kufa - TopicsExpress



          

HIVI TANZANIA BILA USANII HAIWEZEKANI..? Kweli sikio la kufa halisikii dawa labda ndio maana Rais Mwinyi alipoona hatufanikiwi kwenye mchezo wa soka alisema "Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu" Leo gazeti la FAHAMU limeandika "CHEKA APEWA MKANDA FEKI" • Mkanda alioutwaa hautambuliki popote duniani • Bondia aliyepigana nae hajawahi kutwaa taji lolote duniani • Makanda wa Super midle weight aliokabidhiwa Cheka unashikiliwa na bondia wa Australia Sakio Bika na sio Phil Williams kama ilivyodaiwa. UCHUNGUZI Baada ya kusoma habari hiyo nikaamua kudadisi kwa kufuatilia kwenye mitandao mbalimbali ya habari duniani ikiwa ni pamoja na ENEWS, AFP, GOOGLE SEARCH, WIKIPEDIA etc. FINDINGS (Niliyoyagundua ni haya): • Ni kweli Mkanda wa Super midleweight aliokabidhiwa Cheka unashikiliwa na bondia wa Australia Sakio Bika tangu mwaka 2008. Mwaka jana 2012 alitetea taji lake (la Supermiddle weight champion) kwa kumpiga Nikola Sjekloca. • Bondia aliyepigana na Cheka (Phil Williams) ni bondia lakini hakutambulika na Mashirikisho Rasmi ya ndondi duniani kama WBA, WBF,IBF etc . • Amewahi kucheza ndondi lakini hajatwaa ubingwa wowote wa dunia, anatambulika na chama cha ndoni jimbonikwao Minnesota Boxing Association. Amekuwa akicheza mapambano madogomadogo na kabla ya kuja Tanzania alicheza na Charles Goodwin katika ukumbi wa Seven Clans Casino. (Immagine mtu anayecheza kwenye viCassino analetwa Tanzania kama bondia maarufu). • Kazi rasmi ya Phill Williams anayoifanya na inayomtambulisha ni KINYOZI (Barber). Anamiliki saluni yake huko Minneapolis Marekani ambapo anajishughulisha na kunyoa nwele, kusuka, kukata kucha, kupaka rangi etc
Posted on: Tue, 03 Sep 2013 21:12:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015