Habari za Ulimwengu Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya - TopicsExpress



          

Habari za Ulimwengu Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW HABARI | 22.07.2013 | 15:10 Tawi la kijeshi la Hezbollah ni kundi la kigaidi Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana leo kuliorodhesha tawi la kijeshi la Hezbollah kuwa kundi la kigaidi, kwa madai ya kuhusika na mashambulizi barani Ulaya. Muafaka umepatikana, ijapokuwa mawaziri walikabiliwa na upinzani kutoka baadhi ya nchi wanachama kwamba hatua hiyo huenda ikaidhoofisha Lebanon ambako kundi hilo la wapiganaji linatekeleza jukumu kubwa.Kwa kufanya hivyo , mawaziri wamekubaliana kwamba mahusiano ya kisiasa na kiuchumi ya Umoja wa Ulaya na Lebanon yatasalia kuheshimiwa. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle, aliunga mkono hatua hiyo. Uingereza iliwasilisha ombi la kutaka Hezbollah lijumuishwe katika orodha ya makundi ya kigaidi baada kundi hilo la Kishia la Lebanon linaloungwa mkono na Iran kulaumiwa kwa kufanya shambulizi dhidi ya watalii wa Israel nchini Bulgaria na likahusishwa na matukio ya kigaidi nchini Cyprus.
Posted on: Tue, 23 Jul 2013 03:34:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015