Hakuna kitu kibaya kama mtu kukosa utu fadhila ni balaa kubwa - TopicsExpress



          

Hakuna kitu kibaya kama mtu kukosa utu fadhila ni balaa kubwa ndugu zangu, siku zote tumekuwa mstari wa mbele kuwakimbilia wenzetu, na kutoa msaada wa kiutu. Tumekwenda Lebanon, Sudan, Zimbabwe, Eritrea, Liberia, Angola, Mozambique, Seychelles, Uganda, Comoro na sasa Congo, Kagame amesaidiwa hapa hapa Tanzania, pia Museveni huyu hana fadhila hata utu hakumbuki, leo hawa wamegeuka ngombe kutia ulimi puani. Hongera sana JWTZ kwa kazi nzuri mnayoifanya, wanaobeza nawabeze lakini sisi tupo na Jeshi letu na maadamu Serikali hii imechaguliwa na wengi lazima iheshimiwe na kupewa sifa, kukosa uadilifu kwa jeshi la polisi ni jambo jengine sisi tunazungumzia kazi nzuri ya Jeshi letu wanaotaka kuzungumzia ubaya wa jeshi la polisi hapa si pahala pake. Wale wote waliopoteza uhai wao wakiwa katika harakati za kuwakomboa ndugu zetu, hawakupotea bure. Waliojichimbia wakidhulumu rasilimali za nchi ya Congo na kukuza uchumi wao, sasa umefika mwisho wao waafute njia mbadala ya kukuza uchumi na si kudhulumu rasilimali za watu wa Congo, nadhani bado mnakumbuka majeshi ya Uganda na Rwanda walipoamua kwenda kupigana katika ardhi ya Congo, kisa kugpmbania mgao wa mali walizokuwa wakiiba Congo, madhalimu hawa leo wameingana na kuihujumu Congo. Wakongo wana ndugu zao wa kweli nao si wengine bali ni watanzania, wazimbabwe na wasfrika ya kusini. Hureeeee Congo ipo salama sasa!
Posted on: Tue, 05 Nov 2013 14:11:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015