INAWAHUSU WANA NDOA NA WALE WANAOJIANDAA KWA NDOA Dear - TopicsExpress



          

INAWAHUSU WANA NDOA NA WALE WANAOJIANDAA KWA NDOA Dear Friends Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuukwetu sote. “Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangualiponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie.Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tenanikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanzakufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikirinini juu yake. Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwautulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sautiya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike.Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa namaongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujuani nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibuwala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamiakwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Mary. Kwa kwelinilimdharau mke wangu! Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanyakosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepatanyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ilena kuichana vipande vipande. Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali nanguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyowangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalokwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu. Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbuakwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi. Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwakuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kulachakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukuamara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Mary Usiku nilishtuka usingizini mke wangualikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulalatena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochotekutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kablahajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi nayeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana.Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribiakufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirikekisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu,nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbukejinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba nakunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutokakitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwakichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana namasharti yake ya ajabu. NilimsimuliaMary kuhusu masharti yakuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumiaujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa dharau. Mimi namke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwahiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana nakupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yakeyalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafutena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba machona kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka.Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje yanyumba. Alienda kituoni kusubiri basi la kazinikwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwarahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturialiofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mkewangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa namikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembowake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi. Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzikati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwamiaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetuyalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri mweziulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisizaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi. Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi.Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zotezimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyomaana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu anauchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake.Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muendekazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mkewangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendomkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho.Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpakamlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo.Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakiniwepesi wake ulinitia mashaka. Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shidahata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibuna kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zanguofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewatu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Mary alifungua mlangonikamwambia, ‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangaliakwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoamkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki kumtaliki mkewangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wamaisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangunilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu,nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’ Ikawa kama Mary alizinduka usingizini.Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashukangazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengimazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi.Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifokitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu,tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mkewangu kitandani. Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa nasaratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishiaakili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingizekatika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema. Angalau machoni mwa mwanangu naonekana nimume mwema…. Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vyamsingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizokokwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyofuraha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa namwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wauchumba na wa ndoa yenue ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoayenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwakiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao Mungu awabariki nyote mliosoma nakujifunza hapa
Posted on: Mon, 14 Oct 2013 10:26:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015