Ilipoishia, wakati nimelala mida ya saa tisa na nusu za usiku - TopicsExpress



          

Ilipoishia, wakati nimelala mida ya saa tisa na nusu za usiku nilisikia simu inaita...kuangalia nikalia nikakuta yule mwanamke wa kiarabu ananipigia......... Endelea nayo.... Baada ya kujua ni yule mwanamke nilipokea simu na kumuuliza anatake nini usiku ule wa manane, akanambia kuna vitu aliviweka kwa siri kwenye tool box yangu.... Hivyo angependa kunielekeza jambo kuhusu vile vitu alivyoweka kwenye tool box yangu......nikakumbuka kuwa kuna muda nikiwa nyumbani kwake naosha mikono yangu alishika tool box yangu.....nilipo muuliza alidai alikuwa alikuwa ananiwekea vizuri.......baada ya kukumbuka nilimuuliza kwa uoga aliweka nin ndani ya tool box yangu, akanambia kuna tapes za video za siri zinazo uonyesha uozo wa mumewe na cheki ya million ishirin na tano, bastora mbili ambazo takuwa nazitumia kwaajili ya kujilinda,na pia kuna kifurushi cha madini yenye thamani ya million mia tatu....mmmmh! Baada ya kusikia vile usingizi wote ulikata, akaniuliza kama niko jirani na ile tool box ili anielekeze cha kufanya...nikamjibu niliiacha ofisini, akanambia sikutakiwa kuiacha, akanambia natakiwa kuwahi sana ofisini na kuichukua ile tool box bila ya mtu yoyote kujua nini kinaendelea.....akanambia amepigwa sana na mumewe, mumewe anataka kujua nani ameliua joka lake, nikamuuliza kama amemwambia mumewe kuwa mim ndio nimeliua lile joka.....akanambia amemwambia mumewe yeye ndiye aliye liua lile joka...mara ghafla simu ikakata, najaribu kumpigia napata simu yake haipatikani...nachanganyikiwa nisijue chakufanya hata...sikupata tena usingizi kwani nilikua na mawazo mengi juu ya tatizo lililo mfanya yule mwanamke akate simu bila kuniaga....nilikesha nikiwaza atimae kukakucha na makucha yake, asubuhi na mapema huyooo nakawhi ofisini...nikafungua kisha kuangalia tool box yangu pale ambapo huiweka kila siku, ila chaajabu sikuiona...mmmmh nikajaribu kuwauliza wafanyakazi wenzangu wakadai hawajui iliko...nilitafuta sana bila mafanikio hata akili ikachoka.....sijakaa sawa yule mwanamke wa kiarabu ananipia simu...anadai amemtoroka mumewe anakuja kunitafuata nimwambie niko wapi ili tukimbie mji pamoja.....nilikosa cha kumjibu nikaamua kumkatia simu, ile nakata tu yule mzee wa kiarabu akanipia akaniuliza niko wapi, nikamjibu ofisini, akanambia nimsubiri anakuja kisha akakata simu....akili yangu ilichoka kuliko hata nikawa kama chizi.....sijakaa sawa yule mwanamke wa kiarabua ananipigia simu analia sana anadai hatima ya maisha yake iko mikononi mwangu...anaomba nimpatie mzigo wake au nimlinde kwa kila tatizo atalo kabiliana nalo....namkatia simu sijakaa sawa namuona yule mwanamke wa kiarabu anakuja ofisini...nampakia kwenye gari kisiri siri ili mtu yoyote asijue kinacho endelea...wakat tupo njiani gari yetu inapata pancha, tuna simamisha gari kisha tunafungua buti ili tuchukue speya tyre...ile tunafunua tu buti tunakutana na ile tool box...tuanaichua tunafunga tyre kisha hao tunaenda zetu bank kuchukua pesa kwa kutumia ile cheki ya milllion ishirini na tano.....tunafika bank yule mwanamke anaingia kuchukua zile hela...kuangalia pembeni naona gari ya yule mzee wa kiarabu ikiwa barabara ya pili... TUTAENDELEA
Posted on: Tue, 05 Nov 2013 19:42:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015