Jana nilikuwa na rafiki zangu wawili tukijaribu kiichambua siasa - TopicsExpress



          

Jana nilikuwa na rafiki zangu wawili tukijaribu kiichambua siasa ya tanzania,lakin baadaye tukajikuta watu wenye hasira ya kutaka mabadiliko ya nchi yetu kutokana na uzembe wa watu wachache wanaotuongoza. Tulizungumza vitu vingi sana ila cha muhimu ni jinsi mwenyezi Mungu alivyoipendelea nchi yetu kuwa na kila aina ya rasilimali. Ukiangalia nchi kama South Africa imefika leo kama tunavyoiona kutokana na dhahabu pekee,hali kadhalika nchi kama misri,algeria na libya zipo kwenye hatua ya juu katika maendeleo kwa kuwa zina tumia rasili mali zao vizur. Leo hii nashangaa nchi kama Tanzania tunakila aina ya mali kama vile dhahabu,almasi,makaa ya mawe na kadhalika,mungu hakuishia hapo akatupa tanzanite kama katika dunia hii ya duara basi madin haya yapatikane tanzania pekee. hakika tuna bahati ilioje sisi hivi karibuni katupatia gesi,mafuta,uraniam ambazo ni mali muhimu katika kuzalisha nishati hapa nchini. Lakin baada ya miaka 10 tu tunaweza kupoteza kila tulichonacho na kubaki maskini wa milele. Hii inatokana na kutokuwa na viongozi imara wanaoweza kutetea maslahi ya watu wengine,hebu mtanzania mwenzangu funguka na kutetea kizazi kijachopo hata kama utakufa leo hii. naamini jina lako litaendelea kukumbukwa daima. Kwa upande wangu sikubali wawekezaji waje nchini kwetu,NECTA inatuandaa vizuri sana watanzania tunaweza tukafanya mabadiliko ya nchi yetu mwenyewe...jitambue na funguka mtanzania mwenzangu. Jenga kizazi kijacho na siyo maisha yako na familia yako wewe. Naamini tunaweza na tutafanya kitu kwa pamoja
Posted on: Wed, 04 Sep 2013 20:53:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015