Jarida la Ventures financial nchini Nigeria,Limetoa ripoti yake ya - TopicsExpress



          

Jarida la Ventures financial nchini Nigeria,Limetoa ripoti yake ya utafiti juu ya utajiri wa waafrika na kuonesha kuwa Afrika ina watu 55 wenye ukwasi wa pesa,wenye thamani ya dola bilioni 143.88 kila mmoja akiwa na utajiri wa dola bilioni 2.6.Kati ya mabioleana hawa, 20 ni wa Nigeria, 9 kutoka Afrika Kusini, wanane ni raia wa Misri. Kati ya hawa mabilionea wanaoongozwa kwa ukwasi na bilionea aliyekuja kuwekeza nchini kule Mtwara Bwana Aliko Dangote,wamo pia mama yake Rais wa KenyaUhuru Kenyata na Mtoto wa Raisi wa Angola Mwezi Aprili, benki ya dunia ilitoa ripoti yake na kuonesha idadi ya watu wanaoishi katika umaskini mkubwa barani Afrika imeongezeka katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kutoka watu milioni 205 hadi watu milioni 414 . Ukipia tafiti mbalimbali utabaini kuwa wakati idadi ya wenye ukwasi inaongezeka,pia idadi ya watu wanaoishi kwenye umasikini wa kutupwa unakua kwa kasi!watunga sera wetu wakae chini na kulitazama hili,kiwango cha walionancho na wasionancho kinakuwa kwa kasi na kwa pengo kubwa!hii si ishara nzuri kwa amani ya bara la Afrika,wachache kufaidi utajili wa bara hili huku wengi wakitaabika.
Posted on: Tue, 08 Oct 2013 09:15:09 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015