Kikao cha Kamati Kuu kimeisha, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi - TopicsExpress



          

Kikao cha Kamati Kuu kimeisha, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama. Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu. Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.... Tunawapongeza kamati kuu kwa hatua hii muhimu kwa mustakbali wa chama na taifa. UPDATES: Makao makuu ya CHADEMA kufanya press conference na Waandishi wa Habari mchana saa nane.
Posted on: Fri, 22 Nov 2013 12:01:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015