Kinacho shangaza ni hiki kipindi cha dakika 45, nashindwa kuelewa - TopicsExpress



          

Kinacho shangaza ni hiki kipindi cha dakika 45, nashindwa kuelewa kuwa hii ni program ya ITV au ya watu wasioitakia mema Tanzania? Wiki mbili zilizopita tulimshuudia Naibu spika Mh. Job Ndugai akijisafisha juu ya swala la uongozaji Bunge. Wiki iliyofuata tukamshuudia Waziri Mh. Lukuvi nae akimshambulia kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mh. Mbowe. Wiki hii yani jana tumemshuudia Waziri Mh. Wasira akimshambulia Mh. Mbowe na vyama vya Upinzani. Haya ni baadhi tu ya mambo yaliojitokeza katika vipindi vya Dakika 45 ila ndani ya miaka miwili sijawai kuona kipindi hiki kikiwaalika upande wa pili ambao sio Serikali ili kujibu na kutoa ufafanuzi juu ya mambo wanayotuumiwa. Ninavyoelewa Jaji hawezi kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja tu, kwa kawaida mtu anaesikiliza upande mmoja basi huyo moja kwa moja hufanya kazi ya uwakili. Je ITV kupitia kipindi cha dakika 45 kimeamua kufanya kazi ya uwakili kuitetea CCM na kuwakandamiza wengine?
Posted on: Tue, 24 Sep 2013 11:19:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015