MOYO ULIOKUFA: Moyo unapozidiwa na maradhi hufikia daraja ya - TopicsExpress



          

MOYO ULIOKUFA: Moyo unapozidiwa na maradhi hufikia daraja ya kifo, na kifo cha moyo sio kupoteza uhai bali ni kususuwaa na kuwa mgumu, kuwa ni moyo usioathirika, usiowaidhika, na usioogopa. Moyo wa aina hii ndio ule uliosifiwa na Allaah katika Qur-aan pale Aliposema: ثم قست قلوبكم من بعد ذلك فهي كالحجارة أو أشد قسوة..) البقرة 74 ) (Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo; hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi..) 2:74 Moyo uliokufa umeelezwa kwa majina tofauti katika Qur-aan, majina yote yakiwa yanaashiria kususuwaa na kufungika kwa nyoyo kutokana na kuishi katika maradhi kwa muda mrefu bila kupata tiba, mfano tu wa aya zinazoashiria hali hiyo ya nyoyo ni kama zifuatazo: Tuzizingatie 1. Kufungika kwa nyoyo na kutoruhusu mawaidha au nasaha kupenya, Anasema Allaah (Je hawazingatii hii Qur-aan? Au katika nyoyo zao kuna kufuli?) 47:24 2. Nyoyo kupatwa na kutu na kutoathirika kirahisi kwa kutofikiwa na mionzi ya imani, Anasema Allaah: (كلا بل ران على قلوببهم ما كانوا يكسبون) (Sivyo hivyo, Bali yametia kutu ndani ya nyoyo zao maovu waliyokuwa wakiyachuma) 83:14 3. Nyoyo zenye vifuniko au vizibo,nyoyo ambazo hazina tundu wala njia ya kupenyeza mawaidha, Anasema Allaah: (Na walisema nyoyo zetu zimefunikwa (hatufahamu unayoyasema) 2:88 4. Ujinga wa nyoyo na kutokuwa na mazingatio, Anasema Allaah: (لهم قلوب لا يفقهون بها) (Nyoyo wanazo, lakini hawataki kufahamu kwazo) 7:179 5. Upofu wa nyoyo, kutotaka kuona haki na ukweli, Anasema Allaah: (فإنها لا تعمى الأبصار ولكن تعمى القلوب التي في الصدور) الحج 46 (Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyoyo ambazo zimo vifuani ndizo zinazopofuka) 22:46...! Kaka Mkuu #Cable105.
Posted on: Wed, 24 Jul 2013 17:33:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015