MSIBA: ATLANTA, GEORGIA Tumepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba - TopicsExpress



          

MSIBA: ATLANTA, GEORGIA Tumepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa kaka BUYOYA PAUL BISWALO ulitokea huko Atlanta Georgia kwa ajali ya kuzama kwenye maji walipokuwa kwenye (Water Rafting) Jumanne Agosti 6, 2013. Mwili wa marehemu ulipatikana jana Jumatatu Agosti 12, 2013. Marehemu ni ndugu wa karibu wa Familia ya Mwl. Deo Tungaraza., Marehemu alikuwa anaishi mwenyewe huko Atlanta baada ya ndugu zake kurudi nyumbani Tanzania. Kaka wa marehemu anatarajiwa kuwasili muda wowote kuanznia sasa kutoka Tanzania. Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika huko Atlanta, Georgia. Tuikumbuke familia ya marehemu katika sala zetu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana na lihimidiwe. **TAARIFA ZAIDI ZITAFUATA**
Posted on: Tue, 13 Aug 2013 13:04:18 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015